Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo ameungana na wananchi pamoja na viongozi wengine wa kitaifa kote nchini kufanya shughuli za usafi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika.
Dk. Shein alishirikiana na viongozi mbali mbali wa serikali, wananchi, baadhi ya watumishi wa Baraza la Mji wa Zanzibar pamoja na baadhi ya watumishi wa Idara Maalumu za SMZ na vikosi vya JWTZ kufanya usafi katika soko la samaki Malindi mjini Unguja.
Akizungumza mara baada ya shughuli hiyo Dk. Shein aliwakumbusha wananchi haja ya kuimarisha usafi ambao umekuwa ni utamaduni wa watu wa Zanzibar.
Aliwataka wananchi kufanya usafi katika maeneo yote ya kazi, makaazi pamoja na maeneo mengine ili kuimarisha usafi wa mazingira pamoja na wananchi wenyewe kwa kuwa hatua hiyo ni kuimarisha afya zao pia.
“Usafi ndio maisha yetu, ndio afya yetu na ustaarabu wetu hivyo asiyependa usafi hapendi afya yake” alisema Dk. Shein.
Dk. Shein alipongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wa kuitumia siku ya maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu kwa kufanya usafi.
Alifafanua kuwa uamuzi huo ni wa busara na kitendo cha wengine kufanya usafi na wengine kuendelea na majukumu mengine maofisini siku ya leo inadhihirisha umakini na utekelezaji wa kauli mbiu ya “HAPA KAZI TU”
“Tunaungana na wenzetu kuandihimisha siku hii ambayo tumezoea kuiadhimisha kwa gwaride maalum lakini mwaka huu Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Magufuli ametumia busara kuitumia siku hii kuimarisha usafi” Dk. Shein aliwaambia viongozi na wananchi walioshiriki usafi pamoja nae.
Mapema akimkaribisha Mheshimiwa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mhe Haji Omar Kheri alitoa pongezi kwa Dk. Shein kwa kuungana na wanachi pamoja na viongozi katika zoezi hilo la usafi.
Nao wananchi walioshiriki katika zoezi hilo walipongeza juhudi hizo za viongozi wao katika kuthamini umuhimu wa usafi katika maeneo yote nchini hasa ikizingatiwa kuwa kukithiri kwa uchafu ndio kunakosababisha miripuko ya maradhi mbali mbali yakiwemo maradhi ya kipindupindu.
Hivyo wananchi hao walitoa pongezi kwa Rais Dk. Magufuli kwa uwamuzi wake huo wa kuitumia siku ya leo katika kufanya usafi sambamba na kumpongeza Dk. Shein kwa kushirikiana na wananchi pamoja na viongozi katika kutekeleza zoezi hilo la usafi ambapo lina umuhimu mkubwa katika maisha ya mwanaadamu.

No comments:
Post a Comment