WAZIRI Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, ameutaka uongozi wa soko la Kariakoo kufika ofisini kwake Jumatatu ijayo, ukiwa na mikakati ya kuhakikisha soko hilo linakuwa safi muda wote.
Majaliwa alitoa agizo hilo leo baada ya kushiriki kufanya usafi katika soko hilo kubwa kuliko yote nchini lililoko maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam.
Alisema hali katika soko hilo hairidhishi kutokana na kukithiri kwa uchafu na kwamba ni hatari kwa afya ya wafanyabiashara.
Mbali na uongozi wa soko hilo, Majaliwa pia aliutaka uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam, nao kufika ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo.
Alisema licha ya taarifa ya mkuu wa mkoa, Saidi Sadiki kuhusu mikakati waliyonayo kuhusu kuliboresha soko hilo, anataka wakutane kwa pamoja ili kuijadili mikakati hiyo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa alishiriki kufanya usafi kwenye soko hilo, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli, aliyeagiza siku ya leo, ambayo huadhimishwa Uhuru wa Tanganyika, itumike kufanya usafi nchi nzima.
Mara baada ya kuwasili kwenye soko hilo, Majaliwa alipokewa kwa shangwe na wananchi, ambao waliimba nyimbo za kumpongeza huku wengine wakimwita 'jembe, jembe' jembe'
Baadhi ya wananchi walioshiriki kwenye usafi huo walieleza kufurahishwa na agizo hilo la Rais Magufuli na kutaka liwe endelevu badala ya kusubiri Desemba 9 ya kila mwaka.
Wakati huo huo,Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela, amewapongeza watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kuunga mkono agizo la Rais Magufuli la kuigeuza siku ya leo kuwa ya kufanya usafi nchi nzima.
Malecela alisema hayo leo baada ya kushiriki kufanya usafi katika maeneo ya nyumbani kwake, Oysterbay, Dar es Salaam.
Alisema kujitokeza kwa watu wengi kushiriki kufanya usafi nchi nzima ni uthibitisho wa wazi kwamba hakuna lisilowezekana na kutaka zoezi hilo liwe endelevu.

No comments:
Post a Comment