Thursday 24 March 2016

NEC YATANGAZA MAJINA MATATU ZAIDI YA WABUNGE WA VITI MAALUMU

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akitangaza majina ya wabunge wa viti maalumu watatu kuwa ni  Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema). Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kavishe.
 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

IDADI ya wabunge wa Viti Maalum watatu imekamilika baada ya uchaguzi majimbo yote  kufanyika ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata viti maalum viwili na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mmoja.
 

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu ,Damian Lubuva amesema kuwa  uchaguzi umekamilika katika majimbo nane kwa kuwa na majimbo ya Tanzania Bara saba na Zanzibar Moja ambalo ni Jimbo la kijito Upele.
 

Viti vya wabunge wa viti maalum wanatokana na kura za jumla za wabunge wote na kuweza kupatikana viti hivyo.
 

Waliopatikana katika mchanganuo wa viti maalum ni, Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema).
 

Lubuva amesema kuwa kufikia hapo ndipo uchaguzi umekamilika kutokana na viti hiyo kupatikana na kufanya kuwa viti maalumu 113 katika mgawanyo wa viti hivyo ni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Viti  66,  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  viti 35 pamoja na Chama cha Wananchi (CUF)  viti 10.
 

Amesema kuwa kutokana na chaguzi zinazoendelea NEC ndiwe iwe sehemu ya usimamizi wa chaguzi zote.
 

Idadi kura za wabunge CCM katika uchaguzi ambazo zilibaki kutokana wagombea kufariki na kuarishwa kumeongeza viti maalum viwili.

No comments:

Post a Comment