Sunday 20 September 2015

HALIMA DENDEGO AVIASA VYAMA VYA SIASA MTWARA


Na Mwandishi Wetu, Mtwara
MKUU wa Mkoa wa Mtwara Halaima Dendego  ameviasa vyama vya siasa na kuwakikishia wananchi wa Mtawara kwamba kila  mwenye sifa atapata fursa ya kupiga kura bila kubughudhiwa na atakayethubutu kupanga na kuleta ghasia, vurugu atakumbana na mkono wa dola.
Dendego alitoa kauli hiyo jana katika kijiji vjha Mango Panda Nne wilaya ya Mtwara vijijini alipokaribishwa kuwasalimia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kamepni za CCM  iliohutubiwa na Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka mkoani hapa.
Alisema Oktoba 25 mwaka huu Tanzania itawapa fursa wananchi wake kushiriki na kutumia demokrasia ya kuchagua au  kuchaguliwa hivyo kila rai aliyejiandikisha na kuwa mpoiga kura atapata nafasi hiyo na kamwe hakuina wa kumzuia au kumkatazwa asitumie haki yake ya kikatiba na kisheria.
‘Nawaondoa hofu wananchi wote katika Mkoa wa  Mtwara,ifikapo  oktoba 25 kila aliyejiandikisha kupiga kura atatumia haki yake ya kuchagua na kuchaguliwa,nasikia ole wake atakayejiandaa kuleta fujo na wengine kuzuia wenzao wasipige kura, dola ipo na haitakubali amani ya nchi ipotee”Alisema Dendego.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema ni haki ya kila mgomnbea katika kipionddi hiki cha kampeni kunadi sera za chama chake,kuonyesha umahiri na uwezo na umahiri wa kuushwishi na  kuomba kura ili akipata ridhaa aweze kuwatumikia wananchi ipasavyo na si kutoa vitisho,kujenga hasama au kupania shari.
Alisema kiongozi wa chama cha siasa,kundi la watu au mtu atakayethubujtu kufanya fujo na kupandikiza hasama  na chuki kwa wananchi  vyombo vya ulinzi na usalama  vitakimbizana naye kwa miguu mahali popote na  atakapomkamatwa mara moja atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
“Nawatolea wito wazazi muanze kuwaaasa  watoto na  vijana wao,wawaelimisheni  mikono ya dola ni mirefu na ina uwezo wa kumfikia yeyote mahali alipo,muda na wakati wowote ikibidi ,hatutakubali kuiweka nchi yetu rehani na kupoteza amani iliopo”Alisisitiza Dendego.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao wakatambua nao wana wajibu wa kusimaia sheria,kulinda usalama na amani ya nchi na kwamba uchaguzi wa mwaka huu usiwe chanzo cha kuligawa Taifa na kulivuruga.
Alivitaka vyama vyan siasa kujenga nguvu ya hoja kwenye mikutano yao ya kampeni ,kushindaana kwa hoja na sera bila kupigana ,kufanya kamepni za kistaarabu,kwenda na kurudi mikutanoni bila kutumia lugha za matusi pamoja na  kuvumiliana.
“Serikali ya CCM haikuridhia mfumo wa vyama vingi ili watu wapigane makonde ,kutoana ngeu na kuvuruga amani,demokrasias ya vyama vingi ni ushindani wa hoja ,sera na mikakati bila kurupshani,”alisema Dendego.

No comments:

Post a Comment