NA SOPHIA WAKATI, MKINGA
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Mkinga, Dunstan Kitandula, amesema iwapo atachaguliwa kwa mara nyingine kushika wadhifa wa ubunge, atajenga viwanda vidogo vidogo vya kubangulia korosho ili kuharakisha maendeleo ya wananchi wake.
Kitandula (CCM), alisema hayo wakati
akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi
mjini hapa.
Alisema atahakikisha anajenga
viwanda ili kusaidia wakulima wa korosho na kuinua uchumi wa jimbo hilo.
Kitandula alisema viwanda hivyo
vitajengwa katika vijiji vya Mavovo, Horohoro na Mnyenzani na kwamba amefanya
mazungumzo na wawekezaji kwa ajili ya kujenga viwanda hivyo.
Mgombea huyo alisema wanafanya
mazungumzo na kituo cha utafiti wa mbegu za korosho kilichopo mkoani Mtwara ili
wananchi waweze kupata mbegu bora.
Aliwataka wananchi kuwachagua
wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment