Sunday, 27 September 2015

MWILI WA CELINA KOMBANI WAWASILI NCHINI




WAOMBOLEZAJI wakiingiza kwenye gari jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celine Kombani, baada ya kuwasili Uwanj wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, jana. Celine alifariki dunia Alhamisi wiki hiii katika Hospitali ya Apolo, nchini India.

NA REHEMA MAIGALA
MWILI wa aliyekuwa  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina  Kombani umewasiri jana, ukitokea nchini India alipokuwa anapata matibabu katika hospitali Kuu ya Appolo.
Mwili wa Celina ulitua saa 9.45 alasiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, huku ukipokelewa kwa huzuni na viongozi serikali,Bunge, chama,   ndugu ,jamam na rafiki mbalimbali.
Pia mwili wa celina Ulishushwa katika ndege ya Emiretes akitokea nchini humo na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali Kuu ya Jeshi  Lugalo (JWTZ) kwa ajili ya kusubiri taratibu za mazishi.
Akizungumza katika uwanja huo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Ombeni Sefue alisema ,wamepata pigo kubwa kwa msiba wa Celina ambaye alikuwa mchapa kazi hodari na mwanamke anayejali kazi zake kila wakati.
“Serikali tunamlilia na wapiga kura wake pia lakini ni mapenzi ya Mungu yameshatokea hatuna jinsi “alisema Sefue.
Sefue alisema mpaka hivi sasa bado hawajafahamu taratibu za mazishi ,ndio wanakwenda kukaa na familia ili kupanga upya taratibu za mazishi.
“Hivi sasa serikali inakwenda kukaa pamoja na familia ya marehemu Celina ili kujua atazikwa lini na wapi”alisema
Naye, Katibu Mkuu wa CCM Abdulhaman Kinana alisema, CCM imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Mbunge wa Ulanga Mashariki.
“Tulikuwa hatuna wasiwasi wowote na Jimbo la Ulanga kwa sababu tayari wapiga kura wa ulanga walishamkubali Celina kwa kipindi cha miaka 10,na hata uchaguzi wa mwaka huu celina alikuwa bado anashinda”alisema Kinana
Aliongeza kuwa kati wa wabunge waliokuwa wanapigania majimbo yao Celina siwezi kumuacha na ndio maana wapiga kura wake walikuwa wanampenda kwa kila hali.
Wakati huo huo,Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Kailina Ramadhani  lisema  uchaguzi umehairishwa katika jimbo la ulanga mashariki mpaka hapo utakapotangazwa.
Pia alikitaka chama cha CCM kuhakikisha wanapata mgombea kwa kumsimamisha katika jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment