Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi yaviongozi baada ya kuwasili kuanya mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Mkuranga mkoa wa Pwani |
HABARI ZOTE NA ABDALLAH MWERI, KILWA
KATIBU wa Itikadi na Uenezi (NEC) ya CCM, Nape Nnauye,
amesema mwisho wa Chama cha Wananchi (CUF) katika medani ya siasa ni Oktoba 25,
mwaka huu.
Nape amesema CUF itapotea katika ramani ya siasa, baada
ya Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad, kushindwa vibaya katika uchaguzi
mkuu ujao unaotarajiwa kumpata rais wa awamu ya tano.
Katibu huyo alitoa kauli hiyo katika mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, uliofanyika juzi kwenye Kijiji cha Kililima, Kata ya Mingumbi, Kilwa Kaskazini.
Nape alisema Chama cha Mapinduzi kimejipanga kupata kura
za kishindo kwa kuwa mgombea wake wa urais Dk. John Magufuli na Samia ni
wachapakazi hodari.
Alisema CCM itashinda uchaguzi huo licha ya chama hicho kuweka himaya katika mikoa ya kusini na utakuwa mwisho wa Hamad kuendelea na siasa na kutafuta kazi nyingine ya kufanya.
Nape, anayewania ubunge katika Jimbo la Mtama, Lindi aliwataka wakazi wa Kilwa Kaskazini kuondoa hofu kwa sababu CCM imejipanga kushinda baada ya Watanzania kuikubali kutokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
"Mwisho wa CUF ni Oktoba 25, wala msiwe na
wasiwasi, Seif Sharrif Hamad tulianza kumshinda tangu akiwa kijana hadi sasa
amekuwa mzee, CCM imejipanga vizuri na tutapata ushindi wa kishindo,"
alisema Nape huku akishangiliwa na umati wa wakazi wa Kililima.
Alisema kushindwa kwa Hamad katika uchaguzi huo,
kutakiathiri chama hicho Tanzania Bara, kwa sababu hakuna mbunge au diwani wa
CUF ambaye atashinda.
Nape alisema CCM imejiandaa kurejesha jimbo la Kilwa linaloshikiliwa na mbunge wa CUF anayemaliza muda wake, Selemani Bungala 'Bwege'.
"Kuna mtu mmoja anaitwa Bwege hapa Kilwa anatoka Chama cha CUF, safari hii hatoki, tutahakikisha CCM inatwaa majimbo yote, nina hakika tutashinda na mimi nitapiga kampeni mkoa mzima," alisema Nape.
Katibu huyo aliwataka Watanzania kumchagua Dk. Magufuli
kutokana na rekodi yake nzuri ya utendaji katika wizara mbalimbali alizowahi
kuziongoza ikiwemo Wizara ya Ujenzi anayoiongoza.
Alisema Dk. Magufuli amekuwa chachu ya maendeleo ya Tanzania na ametoa rai kwa Watanzania kumchagua sanjari na Samia, ambaye endapo CCM itashinda, ataweka historia kwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais mwanamke.
Pia, Nape alisema Samia ni mtendaji hodari na hana hofu
kuwa atafanya kazi kwa weledi akiwa msaidizi wa Rais katika serikali ya awamu
ya tano.
Katika mkutano huo, Nape alilazimika kusitisha hotuba yake mara kwa mara kutokana na kushangiliwa kwa nguvu na baada ya kumaliza wakazi wa Kililima walimtaka kuendelea
No comments:
Post a Comment