Thursday, 1 October 2015

'DK. MAGUFULI NDIO TIBA YA TATIZO LA AJIRA'




Na Mwandishhi Wetu, Wete


UMOJA wa Vjana wa Chama Cha Mapinduzi umesema tatizo la ajira kwa vijana linaloikabili nchi litafikia tamati ikiwa vijana watamchagua mgombea urais  kupitia CCM Dk. John Magufuli.

Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo jana katika mkutano wake na makundi ya vijana wa CCM, kwenye ukumbi wa Jamhuri, Wete  Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Shaka alisema ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 imeainisha hatua mbalimbali itakazozichukua kuhakikisha tatizo la ajira linapatiwa ufumbuzi.


Alisema miongoni mwa mikakati itakayotumika kukabiliana na tatizo hilo ni pamoja na kufufua mashirika ya umma, ujenzi wa viwanda vidogo vya kati na vikubwa pamoja na kujenga reli mpya itakayochochea shughuli za kiuchumi kwenye maeneo mbalimbali ya nchi.

 
"Ilani ya uchaguzi anayoinadi mgombea urais wa CCM Dk. Magufuli ndiyo yenye majibu na utatuzi wa changamoto ya ajira kwa vijana. Miongoni mwa mikakati yake ni kufufua viwanda, ujenzi wa reli na bandari, ambavyo kwa pamoja vitahitimisha kilio cha ajira nchini," alisema shaka.


Alisema kwa upande wa Zanzibar, mikakati ya kuongeza ajira kwa vijana itazingatia mazingira maalum ya fursa za uchumi  visiwani humo.

"Katika kupambana na changamoto ya umasikini , CCM itazielekeza serikali zake kuboresha maisha ya wananchi wote, hususan vijijini kwa kuchukua hatua mbalimbali,” alisema.

Hata hivyo, akiwaeleza vijana kuwa tayari  kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa, huku akisema kuwa kitendo cha kupoteza wakati kwa kutegemea ajira katika sekta ya umma  kisiwe katika vichwa vya vijana, badala yake wanatakiwa kujikita katika sekta binafsi.

"Asije mgombea yeyote wa nafasi yoyote akakudanganyeni kwamba ana uwezo wa kutoa ajira kwa vijana wote wa Zanzibar kwenye utumishi wa umma ,hilo halowezekani,” alisema.

No comments:

Post a Comment