Na Chibura Makorongo, Simiyu
POLISI mkoani
Simiyu imethibitisha kutekwa kwa mgombea ubunge jimbo la Bariadi kwa tiketi ya ACT
Wazalendo, Masunga Ng’hozo.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemini
Mushy, alisema tangu kutoweka kwa mgombea huyo, simu yake imekuwa ikitumika
kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa wazazi wake.
Alisema ujumbe
huo umekuwa ukiwataka wazazi wake kutoa kiasi cha fedha sh. milioni 2.5 ndipo mgombea
huyo aachiwe huru, vinginevyo wajiandae
kupokea maiti.
Ng’hozo,
ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino
(SAUT), tawi la Mbeya, alitoweka Septemba 27, mwaka huu, akitokea katika ofisi
ya chama hicho mkoani hapa.
Alisema
polisi walipata taarifa za kutekwa kwa mgombea huyo Septemba 29, mwaka huu, ambapo
alieleza mpaka sasa hajulikani alipo.
No comments:
Post a Comment