WATU wawili akiwemo mwanasheria Angela Mbonde, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shitaka la kula njama ya kumuua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva na familia yake.
Angela (36), mkazi wa Sinza na Samwel Gitaro au Koroso (30), ambaye ni mwalimu na mkazi wa Ukonga Kipunguni, Dar es Salaam, walifi kishwa mahakamani hapo jana.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hellen Moshi, aliwasomea washitakiwa hao shitaka la kula njama ya kumuua Jaji mstaafu huyo na familia yake.
Hellen alidai washitakiwa hao walitenda kosa hilo, kati ya Oktoba 25 na Novemba 6, mwaka huu, sehemu tofauti za mji wa Dar es Salaam na mahali pengine katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alidai washitakiwa hao kwa pamoja walikula njama na watu wengine ambao hawakuwepo mahakamani kumuua Jaji mstaafu Lubuva na familia yake.
Washitakiwa hao ambao walikuwa wakitetewa na Wakili Mosses Karua kwa niaba ya Wakili Peter Kibatala, walikana shitaka hilo, ambapo Wakili Hellen alidai upelelezi haujakamilika na kuomba kupangiwa tarehe nyingine ya kutajwa.
Wakili Karua aliiomba mahakama kuwapatia washitakiwa dhamana kwa kuwa shitaka linalowakabili linadhaminika kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, Wakili Hellen alidai upande wa Jamhuri unatambua shitaka hilo lina dhamana kisheria, lakini wanaomba dhamana ya washitakiwa ishikiliwe kwa muda.
“Tunaomba dhamana ya washitakiwa ishikiliwe kwa muda kutokana na uhalisia wa kosa lenyewe na hatua za sasa za upelelezi, hawapaswi kupewa dhamana mpaka tutakapoona inafaa kupewa dhamana,” aliomba Hellen.
Kwa upande wake, Wakili Karua alidai sababu za upande wa Jamhuri za kuzuiwa kwa dhamana ya washitakiwa hazina msingi kisheria, suala la msingi la kujiuliza kesi inadhaminika.
Alidai mambo mengi ya hisia yanapaswa kuthibitishwa kwa kiapo, hivyo anaomba washitakiwa wapewe dhamana kwa masharti yatakayotolewa na wapo tayari kuyatekeleza.
Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Simba alisema licha ya kwamba kosa linadhaminika anakubaliana na hoja za upande wa Jamhuri, hivyo washitakiwa walikataliwa dhamana.
Hakimu Simba aliutaka upande wa Jamhuri kuhakikisha upelelezi unakamilika mapema na kusema washitakiwa watakwenda rumande hadi Desemba 15, mwaka huu, kesi itakapotajwa.

No comments:
Post a Comment