Saturday, 30 January 2016
UANZISHAJI WA MAHAKAMA MAALUMU YA MAFISADI UMEFIKA PAZURI
SERIKALI imewahakikishia Watanzania kuwa mchakato wa kuanzishwa kwa mahakama maalumu ya mafi sadi na wezi,
umefika hatua nzuri.
Aidha, imesema ukiachia hotuba ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hotuba ya Rais Dk. John Magufuli, aliyoitoa wakati akizindua Bunge ni bora kuliko hutoba nyingine zote.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema hayo juzi bungeni mjini hapa wakati akichangia hotuba ya Rais.
Akizungumzia mchakato wa kuanzishwa kwa mahakama maalum ya mafi sadi na wezi, alisema unakwenda vizuri na utakapokamilika Watanzania watafahamishwa.
"Kiongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, akitoa tamko lazima litekelezwe," alisema.
Kama tunakumbuka Rais, kwa nyakati tofauti kipindi cha kampeni aliahidi kuanzisha mahakama maalumu ya mafi safi na wezi.
Akizungumzia hotuba ya Rais, wakati wa ufunguzi wa Bunge, alisema ukiacha hutoba ya Mwalimu Nyerere, hotuba ya Rais Magufuli nayo ni bora kuliko za viongozi wengine wote.
Dk. Mwakyembe alisema hotuba hiyo iligusa mioyo ya Watanzania wenye nia njema na taifa.
Wakati Rais, anatoa hotuba yake iliyokuwa na aya 160, alipigiwa makofi na vigelegele mara 137 ni zaidi ya asilimia 86, ya Martine Luther ambaye ni Mmarekani mweusi.
Alisema hotuba hiyo imewaweka pabaya wapinzani waliokuwa wanapinga kila kitu.
Dk. Mwakyembe alisema tatizo la hotuba hiyo kwamba ukijaribu kuipinga wananchi watakuona wa hovyo.
"Wamejaribu kutoka kwenye mjadala kwa hoja tu ya TBC (Shirika la Utangazaji la Tanzania) ili wasiwepo kwenye mjadala kwani wakiwepo lazima wataisifi a tu," alisema.
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, alisema sekta ya viwanda inatoa ajira kubwa na kwamba kila mkoa umeelekezwa kujenga kiwanda.
Alisema viwanda vilivyopo nchini, watahakikisha vinafanya kazi na vitaondoa vikwazo vilivyopo.
Mwijage aliwataka wawekezaji wawekeze kwa kutengeneza ajira nyingi ili waweze kuchangia kulipa kodi.
Akizungumzia viwanda vilivyobinafsishwa, aliwataka waliopewa viwanda hivyo wajisalimishe na waeleze wanavifanyia nini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema wizara yake itahakikisha umeme unapatikana kwa wingi.
Alisema katika kipindi cha miaka miwili na nusu, asilimia 67 ya vijiji vyote nchini, vitapata umeme.
Naye, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, alisema huu ni wakati wa vijana kutoka mijini kwenda vijijini kwani huko ndiko kwenye mali.
Alisema wizara inatarajia kutenga maeneo maalumu ya ufugaji na kuweka miundombinu kwa lengo la kupunguza migogoro ya wafugaji na wakulima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment