Thursday 26 May 2016

DK. SHEIN ZIARANI COMORO


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, anaondoka leo jioni kwenda Muungano wa Visiwa vya Comoro kwa ziara ya siku mbili.
 

Akiwa nchini humo, Dk. Shein atamwakilisha Rais Dk. John Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Azali Boinakher.

Kuapishwa kwa Boinakher kunafuatia ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika Aprili 10, mwaka huu  na ule wa marudio katika kisiwa cha Anjouan, uliofanyika Mei 11, 2016.

Sherehe za kuapishwa kwa rais huyo mteule zitafanyika kesho katika kiwanja cha mpira cha mjini Moroni na zinatarajiwa kuhudhuriwa viongozi mbalimbali kutoka nje ya nchi hiyo.

Katika ziara hiyo Dk. Shein amefuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi Gavu na Mshauri wa Rais Uhusiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa.

Dk. Shein  anatarajia kurejea nchini kesho mchana.

No comments:

Post a Comment