Sunday 1 May 2016

VYAMA VYA UPINZANI VIPO ICU- SHAKA



Na Woinde Shizza , Kilimanjaro

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umesema muda mfupi ujao  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kitaifuata mahali viliko   vyama vya  NCCR-Mageuzi, TLP na Chama cha Wananchi  (CUF ) kwa sababu kimejidhuru kukubali   kukumbatia mafisadi .

Aidha umoja huo umevitaja  vyama hivyo sasa  vinachechemea, vinaishi kwa matimaini   na viko mahututi kwani  wakati wowote  , ugonjwa uliovitafuna vyama hivyo utakishambiulia  chadema.

Matamshi hayo  yametamkwa leo na  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM  Shaka Hamdu  Shaka wakati akizungumza na wanachama wa Uvccm na jumuiya zake katika mkutano wa hadhara  uliofanyika katika kijiji cha Maendeleo Kata ya Mabogini wilaya ya Moshi vijijini.

Shaka alisema jeuri na mbwembwe za NCCR ‘Mgeuzi, CUF na TLP muda  umepita na sasa havina mategemeao tena ya kuibuka na  kushindana na chama tawala .

Alisema vyama hivyo hupenda  kujiita vyama  vya siasa jambo ambalo alisema si kweli kwasababu kujiendesha kwake kunamtegemea mtu badala ya kujijenga na kuwa taasisi kamili.

Alisema vyama hivyo vineajua kutegemea makapi yaloachwa  na ccm  ili yawasaidie kuendesha masuala ya kisiasa .

Shaka akizungimza katika mkutano huo alimtolea  mfano mbunge wa Moshi vijijini Anthony Komu (chadema)  akisema hana uwezo wala uaminifu katika dhima ya kuwatumikia wananchi kwasababu historia yake ya kisiasa haionyeshi kama mtu madhubuti  na mwenye msimamo.

“Komu alikuwa mwanachama na kiongozi wa NCCR -Mageuzi tokea mwaka 1992 , akahama na kujiunga Chadema akivutiwa na ukabila, wakati fulani akataka aende TLP  Mrema akamuwekea ngumu   , aina ya kiongozi kama Komu ni ushahidi tosha si kiongozi  muaminifu ,  kesho  sivajabu ukasikia amegama chadema kurudi ccm  “alisems Shaka

Hata hivyo Kaimu huyo katibu Mkuu aliitaka halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini kufanya kila linalowezekana kupekeka maji katika maeneo ya kata ya Mabogini ili wananchi waondokane na  adha ya ukosefu maji.

“Wananchi wa Moshi vijijini nakuhalikishieni  kuwa ujenzi wa barabara yenu umbali wa kilomita 14 toka TPC hadi Chekereni itatekelezwa na serekali ya  Dk Magufuli kwa kiwango cha lami  “alisema shaka.

Katika kijiji cha Chekereni kata ya mabogini  wanachama wapya 34 wamejiunga na Uvccm, 27 CCM na UWT wanachama 12.

No comments:

Post a Comment