CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimefichua mkakati wa siri uliojifi cha nyuma ya operesheni mpya ya CHADEMA, waliyoiita UKUTA kuwa inafadhiliwa na wakwepa kodi na wahujumu uchumi waliobanwa mianya yao.
Mpango huo ulifi chuliwa jana na Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, katika mkutano wake na waandishi wa habari, ambapo alisema operesheni hiyo inalenga kumdhoofi sha Rais Dk. John Magufuli katika utendaji kazi wake madhubuti.
Sendeka alisema tamko lililotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kama maelezo ya maazimio ya Kamati Kuu ya Chama hicho, imejaa uongo na ghiliba nyingi za kibabaishaji.
Alisema kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli ni kubwa na wapinzani wamekosa agenda na ndio maana wanakuja na operesheni zisizokuwa na faida kwa taifa huku wakiwa wanawatetea wahujumu uchumi na wakwepa kodi.
“Wapinzani wanataka kutunga uongo ili waendelee kupata wafuasi, huku wakijua fi ka serikali haijazuia mikutano ya kisiasa, kwani wabunge wapo huru kufanya mikutano kwenye majimbo yao yote, lakini tunajua wanataka kuwatetea wahujumu uchumi na wakwepa kodi,” alisema.
Msemaji huyo wa CCM alisema lazima Watanzania waelezwe ukweli kuwa hoja za wapinzani sio za kweli na wanapaswa kujiuliza udikteta wa Rais Dk. Magufuli ni kuzuia na kuwashughulikia watumishi hewa, kuwabana wakwepa kodi, kupunguza na kudhibiti safari za nje, au kubana matumizi ya serikali.
Alisema CCM inaamini Watanzania wengi wanaunga mkono juhudi za Rais Dk. Magufuli na hawatakuwa tayari kuona damu za Watanzania zikimwagika kutokana na uongozi wa watu wachache, wanaotumia siasa kumwaga damu za Watanzania wasiokuwa na hatia.
“CCM inapenda kuwaasa Watanzania wajiulize maswali ya msingi kabla ya kushiriki. Ni vizuri watafakari na kujiuliza maswali ya msingi kabla ya kuamua kushiriki au kuruhusu watoto wao kuwa mbuzi wa kafara,’’alisema.
Ole Sendeka alisema maandamano yeyote yana madhara makubwa, hivyo Watanzania wasiendelee kukubali kuwa mbuzi wa kafara kutokana na ulafi wa watu wachache, wanaoamini kufanya mambo maovu ili kujipatia madaraka.
Msemaji huyo alisema hakuna operesheni yeyote iliyofanywa na CHADEMA, ikiwa na mafanikio na kuwasaidia Watanzania wa kawaida, zaidi ya kujenga umaarufu wa viongozi wachache wa chama hicho na kuneemesha matumbo yao na kupoteza maisha ya watanzania.
CCM HAIOGOPI MIKUTANO YA HADHARA
Akizungumzia kuzuiliwa kwa mikutano ya kisiasa na serikali, Ole Sendeka alisema CCM kila siku inakaa
na kuomba mikutano hiyo iruhusiwe kwa kuwa wana mambo mengi ya kuwaeleza Watanzania juu ya utendaji kazi wa Dk. Magufuli.
Alisema CCM haiogopi mikutano ya hadhara, ndio maana kabla haijasitishwa ilishatoa mwelekeo wa ratiba yao ya mikutano, kwa kuwa Katibu Mkuu, Msemaji wa Chama na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM wote walikuwa na ziara za kichama mikoani, lakini waliahirisha.
Juzi, katika mkutano na waandishi wa habari, Mbowe alisoma tamko la Kamati Kuu ya Chama hicho huku akidai kuwa kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu, wanaanza mikutano ya hadhara nchi nzima kwa madai kuwa wanapinga udikteta unaofanywa na serikali huku wakitoa hoja dhaifu zisizokuwa na mashiko kwa jamii.

No comments:
Post a Comment