Wednesday 16 September 2015

WEMA SEPETU AIPASUA UKAWA




NA ABDALLAH MWERI,LINDI
MSANII nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu, amepasua jipu na kusema Umoja wa Vyama vya Upinzani (UKAWA), ulitaka kumuhonga dola 50,000.
Wema aliyasema hayo jana katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Hassan, uliofanyika  kwenye Uwanja wa Nyangao, Lindi.
Nyota huyo aliyeongozana na wasanii nyota wa filamu nchini, alisema viongozi wa UKAWA walimfuata na kumtaka kuihama CCM baada ya kushindwa katika kura za amaoni alipowania viti maalum mkoani Singida.
Alisema siku moja baada ya kufanyika uchaguzi huo, alipigiwa simu na kigogo mmoja wa UKAWA (jina kapuni kwa sasa), na kumuahidi dola 50,000 na ubunge kupitia umoja huyo.
Alisema alimjibu kigogo huyo na kumwambia hataihama CCM na hadanganyiki na kusema hawezi kuihama CCM kwani baba yake aliwahi kuwa waziri katika serikali ya Zanzibar.
Wakati huo huo, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Snura Mushi, jana alizikonga nyoyo za wakazi wa Mtama baada ya kutoa burudani kali iliyowachengua maelfu ya wakazi wa jimbo hilo waliojitokeza katika mkutano wa kampeni.

No comments:

Post a Comment