Wednesday 16 September 2015

KIWANDA CHA KOROSHO MTAMA KUFUFULIWA


Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, akihutubia mkutano wa kampeni katika Jimbo la Mtama.
Mgombea wa ubunge Jimbo la Mtama na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye akizungumza na wapiga kura wake katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa wamefurika katika viwanja vya Nyangao Jimboni Mtama katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza

SERIKALI ya awanu ya tano inatarajia kufufua kiwanda cha korosho kilichopo jimbo la Mtama, mkoani hapa.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni, mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, alisema ujenziwa kiwanda hicho utaanza mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani.
Samia alitoa ufafanuzi huo, baada ya kuombwa na mgombeaubunge jimbo la jimbo hilo kupitia CCM, Nape Nnauye.
Alisema kiwanda cha korosho kitakuwa na manufaa kwa wakazi wa mikoa ya lindi na mtwara ambapo zao hilo la biashara limekuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi.
'Nimesikia ombi la mbunge wenu mtarajiwa, tupeni mwaka mmoja tutakifufua kiwanda cha korosho' alisema Samia.
Pia Samia alitoa onyo kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika wasiokuwa waaminifu wajiandae kutafuta kazi zingine.
Alisema vyama vingi vya ushirika vimekufa kutokana na utendaji mbovu wa viongozi, lakini serikali ya awamu ya tano itawaondoa katika nyadhifa zao bila kuwaonea haya.
“Wakuu wa vyama vya ushirika wazembe tuwashughulikia, wamepewa uongozi kuwatumikia wakulima si kunenepesha matumbo yao” alisema Samia kwa sauti ya ukali.
Wakati huo huo, mgombea mwenza huyo alisema jimbo la Mtama linapaswa kuwa wilaya mpya kutokana na wingi wa wakazi wake.
Samia aliwataka viongozi wa jimbo hilo kufuata utaratibu wamaombi na yakifika mezani kwake atafanyia kazi ili Mtama iwe wilaya mpya.
Awali, Nape alisema, jimbo la Mtama lina kata 20 na wakazi wake wanafuata huduma zote muhimu Lindi mjini.
Nape alisema wakazi wa jimbo hilo wameshindwa kupata maendeleo kutokana na kukosa huduma muhimu za kijamii.
Pia alisema wakazi hao wanabiliwa na umasikini unaotoka nakukosa umeme ambo ni chanzo cha kuzalisha ajira kwa vijana na wanawake.
“Mama wakazi wa mtama wana matatizo makubwa sana, hawana umeme na maji ktk vijiji vingi” alisema nape
Nape ambaye ni katibu wa NEC, itikadi na uenezi ya CCM, alisema wakazi wa mtama wana changamoto ya kukosa soko bora la mazao ya korosho na ufuta.
Akijumuisha maombi ya Nape, mgombea mwenza alisema serikali ya dk john magufuli itafanyia kazi kwa kuwa yamo katika ilani ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment