Saturday 30 July 2016

PAPA FRANCIS AANGUKA GHAFLA WAKATI AKIENDESHA MISA


WARSAW, Poland

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ameanguka ghafl a wakati akiongoza misa baada ya kujisikia vibaya nchini Poland.

Habari zilizotangazwa na vyombo vingi vya habari duniani vya kimataifa jana, zilisema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76, huwa anasumbuliwa na tatizo la maumivu ya miguu na mgongo.

Ilielezwa kuwa kiongozi huyo alianguka katika misa iliyokuwa ikifanyika Czestochowa, Poland wakati akianza kuwaombea watu waliofurika kwenye uwanja huo.

Habari zilisema baada ya kuunguka, alipewa msaada wa kwanza na wasaidizi wake alioambatana nao kwenye ziara yake nchini Poland.

Kiongozi huyo alikuwa na ziara ya siku tano nchini Poland katika mji wa Czestochowa, ambao upo kusini mwa nchi hiyo kwa ajili ya maombezi.

Habari zaidi zilisema eneo aliloanguka kiongozi huyo ni takatifu, ambapo kumekuwa kukitokea miujiza.

Papa alikosea kushuka ngazi, ndipo akaanguka wakati akienda kwenye eneo takatifu la Jasna Gora. Hata hivyo, hakupata majeraha yeyote baada ya tukio hilo.

No comments:

Post a Comment