RAIS Dk. John Magufuli, amemwagiza Inspekta Jenerali wa Polisi nchini kuwaondoa wafanyakazi raia waliopo katika jeshi hilo, hususani wasio na tija, ili kuruhusu shughuli zote kufanywa kwa uadilifu na askari wenyewe wenye taaluma husika.
Vile vile, ameagiza kukamatwa kwa mzabuni aliyepewa kazi ya kutengeneza sare za jeshi hilo na kukabidhiwa takribani sh. bilioni 60 ndani ya wiki moja na kutokomea.
Rais Magufuli, ameahidi kuendelea kuboresha maslahi ya askari, ikiwemo mishahara na makazi, licha ya kuwaongezea posho kwa kufuta maduka yaliyokuwa na misamaha ya kodi.
Hata hivyo, amelipongeza jeshi hilo kwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa uhalifu wa kutumia silaha na kusisitiza kuhakikisha wanawanyang’anya silaha majambazi kabla hawajaleta madhara.
Rais Magufuli, alisema hayo jana, Ikulu, jijini Dar es Salaam, wakati wa kuapishwa makamishna waandamizi wasaidizi wa polisi 23 na manaibu kamishna aliowateua mwishoni mwa wiki.
“Kwa kutambua kazi kubwa mnayofanya, miezi kadhaa iliyopita nilimwagiza IGPkuwatafuta ambapo aliangalia historia na kazi zenu, yalikuja majina mengi, SACP walikuwa 31 mikawarudisha 23 tu na DCP walikuwa 46 na wamerudi 35 tu, ninyi ndio mnastahili,” alisema Magufuli.
Aliongeza kuwa alipata habari zote za watu ambao hakuwapitisha, hivyo wamepewa muda wa kujirekebisha.
“Nalipongeza kwa dhati Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri na kubwa mnayofanya ya kulinda usalama wa raia na mali zao, ushahidi upo, ni jinsi mlivyosimamia kikamilifu mchakato mzima wa uchaguzi mkuu, mwaka jana, bahati nzuri mnazijua na kuzisimamia sheria,” alisema Magufuli.
Aliwataka kuwaacha askari kufanya kazi zao kikamilifu na kutolea mfano kuwa awali askari waliadhibiwa walipowakamata magari ya baadhi ya vigogo, aliwataka kuwapa mamlaka ya kutekeleza kikamilifu wajibu wao.
“Hata iwe gari ya IGP, RPC, waziri au rais, wakamate na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, mhusika atajitetea mwenyewe huko baadaye,” alisema.
Aliwataka kuweka vyeo vyao pembeni na sheria mahali pake, ili kuwapa nguvu wale wanaowaongoza kwa kuwa askari wanaofanya kazi vizuri ni mwengi, licha ya wachache wanaoharibu.
Aliwataka kwenda kufanya kazi zao kwa nguvu zote wakimtanguliza Mwenyezi Mungu, huku wakitimiza wajibu wao kama walivyoapa.
Rais, aliwataka viongozi hao kujenga umoja, kupendana na kuacha kupigana vita na fi tina, kwa kuwa anazo baadhi ya taarifa hizo.
“Ninyi ni chombo cha baba mmoja, mmelelewa katika maadili sawa, mkawe wamoja, taifa linawategemea kusimamia mambo kikamilifu, mkitetereka, nchi itatetereka, nawaombea mafanikio na watakaowakamisha wakwame wao,” alisema.
KUNDOLEWA RAIA NDANI YA POLISI
Alisema hatua ya kupunguza raia wanaofanya kazi katika jeshi la polisi, inafuatia utovu wa nidhamu wanaoufanya, ambapo jeshi hilo hushindwa hata kuwapa adhabu za kijeshi kwa kuwa wao ni raia. Dk. Magufuli alitolea mfano wa ubadhirifu uliokuwa ukifanywa na mhasibu wa jeshi hilo.
“Ninyi ndio mnakamata wahalifu hadi wanaoiba kuku, leo mnashindwa kumkamata mwizi mliye naye ndani, IGP, DCI, makamishna, wote mpo hapo hapo lakini mnashindwa kumbaini! Alionyesha kushangaa
Aliagiza wafanyakazi raia watakaopunguzwa katika jeshi hilo kuhamishiwa Idara ya Utumishi ili kupangiwa kazi maeneo mengine, badala ya kukaa na kulichafua jeshi hilo na kazi walizokuwa wanafanya kupatiwa askari wenye taaluma husika.
“Kwa nini mnakaa na raia? Mengine mnayatafuta wenyewe, chombo hiki ni muhimu katika nchi, pale inapojitokeza dosari ni lazima ikashughulikiwa haraka,” alisema.
Aliwasisitiza kufanya kazi zao wenyewe, ili wanapobainika wanaokosea washughulikiwa kijeshi.
“Ninyi ni chombo cha baba mmoja, mmelelewa katika maadili sawa, mkawe wamoja, taifa linawategemea kusimamia mambo kikamilifu, mkitetereka, nchi itatetereka, nawaombea mafanikio na watakaowakamisha wakwame wao,” alisema.
KUNDOLEWA RAIA NDANI YA POLISI
Alisema hatua ya kupunguza raia wanaofanya kazi katika jeshi la polisi, inafuatia utovu wa nidhamu wanaoufanya, ambapo jeshi hilo hushindwa hata kuwapa adhabu za kijeshi kwa kuwa wao ni raia. Dk. Magufuli alitolea mfano wa ubadhirifu uliokuwa ukifanywa na mhasibu wa jeshi hilo.
“Ninyi ndio mnakamata wahalifu hadi wanaoiba kuku, leo mnashindwa kumkamata mwizi mliye naye ndani, IGP, DCI, makamishna, wote mpo hapo hapo lakini mnashindwa kumbaini! Alionyesha kushangaa
Aliagiza wafanyakazi raia watakaopunguzwa katika jeshi hilo kuhamishiwa Idara ya Utumishi ili kupangiwa kazi maeneo mengine, badala ya kukaa na kulichafua jeshi hilo na kazi walizokuwa wanafanya kupatiwa askari wenye taaluma husika.
“Kwa nini mnakaa na raia? Mengine mnayatafuta wenyewe, chombo hiki ni muhimu katika nchi, pale inapojitokeza dosari ni lazima ikashughulikiwa haraka,” alisema.
Aliwasisitiza kufanya kazi zao wenyewe, ili wanapobainika wanaokosea washughulikiwa kijeshi.
KUBORESHA MASLAHI YA ASKARI
Rais Magufuli, aliahidi kuendelea kulinda na kuboresha maslahi ya askari, ikiwemo mishahara na makazi, licha ya kuwaongezea posho.
Alisema, hatua ya kuwaongeszea posho ilitokana na kufutwa kwa maduka yaliyokuwa na misamaha ya kodi ambapo fedha hizo zitawasaidia kufanya manunuzi.
“Tunakusudia kufanya marekebisho ili kuboresha jeshi, tutawapatia makazi polisi, magereza, zimamoto kama tulivyofanya kwa JWTZ na usalam,” alisema.
UKUSANYAJI WA KODI
Rai Magufuli, alilipongeza jeshi hilo kwa kazi nzuri ya kukushanya kodi inayofanywa na jeshi hilo katika kuchangia pato la taifa.
“Baadhi ya watu wanalalamika hivi sasa meli zimepungua bandarini, zilikuwa hazilipi kodi, bora ziache kabisa kuja, badala ya kuja na kutolipa, nataka zikija zilipe,” alisema.
Vile vile, alisema suala la watalii kulipa VAT ni lazima, tofauti na malalamiko kuwa watapungua kuja kutalii nchini, alisema ni bora waje wachache walipe kuliko wengi wasiolipa.
Alisema ufujaji wa fedha za serikali ulikuwa mkubwa kiasi cha watu kwenda kula ‘wikiendi’ Dubai, pia yapo malalamiko nyumba sinza zimekosa wapangaji kwa kuwa mtu mmoja aliweza kupangishia nyumba toifauti watu kadhaa.
“Hakuna haki ya watu kufurahia maisha maisha na wengine kuteseka, watu wote wanapaswea kufaidi matunda ya nchi yao,” alionya Magufuli.
Aliwataka kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha ili zinazopatikana zitumike kwa manufaa ya umma maeneo mbalimbali.
UHALIFU WA KUTUMIA SILAHA
Alilipongeza jeshi hilo kwa suala la ulinzi na usalama hususani katika vituo vya polisi unaofanywa hivi sasa.
“Sijasikia kwa kuda sasa kuvamiwa kwa kituo chochote cha polisi na askari kuuawa bila wavamizi kunyang’anywa silaha zao,” alisema.
Alisema, anaamini uhamisho wa makamanda wa mikoa alioufanya, umechangia kwa kiasi kikubwa hali hiyo kwa kuwa wamekwenda kufanya kazi kikamilifu.
Alisema, pamoja na kazi nzuri wanayowanya bado wapo askari wachache wanaolichafua jeshi hilo kwa maslahi yaona nia mbaya waliyo nayo.
“Nawaagiza mkawaeleze kuacha tabia hizo ikiwezekana kuwaomndoa kabisa kazini, ni wachache sana kiasi cha asilimia 0.0001 hawana sababu ya kulichafua jeshi,” alisema Rais Magufuli.
Alisema, dunia sasa hivi imebadilika, wasiendekeze suala la ‘polisi jamii’ lazima raia amwogope askari.
“Majambazi wanavamia vituo, polisi wanaangalia tu, eti polisi jamii, wanyang’anyeni, kwani sheria inasema polisi wanyang’anywe silaha?” alihoji Magufuli.
Katika hali isiyo ya kawaida kwa rais, katika hafl a hiyo, Magufuli, alibeba sahani na kuwagawia wageni waalikwa vitafunwa na vinywaji, jambo lililofanya kila mtu kufurahi na kupiga kofi .
MwiguluWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, aliwataka makamishna hao kuhakikisha wanashughulikia masuala yanayojitokeza mapema kabla hayajachafua Jeshi la Polisi.
”Ninyi ni wasaidizi wa ngazi ya juu yaani serikali, mnapaswa kuwa waadilifu na kushughulikia mambo mapema, siyo mpaka ngazi za juu watambue na ndio ninyi mmshughulikie,” alisema.
Alisema tatizo la raia kujichukulia sheria mkononi, linatokana na wahalifu kukamatwa mara kadhaa na kuachiwa, aliwataka kukomesha suala hilo na kuwachukulia hatua stahiki wahalifu hao.
Jaji Salome Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu, Salome Kaganda, kabla ya kuwawapisha makamishna hao, aliwataka kuunda kamati za maadili katika ngazi zote kuanzia wilaya, ili kushughulikia matatizo, badala ya kumwachia IGP jukumu hilo.
“Kamati hizo zinapaswa kuwasikiliza kikamilifu askari badala ya kuwaonea, askari hupata mfadhaiko na kuamua kumalizia hasira zao kwa wananchi, wasikilizwe na kutatuliwa kero zao,” alisisitiza Jaji Salome.
Aliwataka kuhakikisha wanatekeleza waliyoahidi. Kwa upande wake, Insekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu, aliwataka askari kuwajibika kikamilifu, vinginevyo watakaoharibu watanyang’anywa vyeo vyao.
Naye Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju, alisema jeshi ni kiungo muhimu kwa nchi na ndio serikali, ili shughuli nyingine hususani za kijamii kufanyika vizuri, jukumu la serikali ni kudumisha amani ya nchi.
No comments:
Post a Comment