Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, mbunifu wa mavazi na mwanamuziki , Jokate Mwegelo kwa kushirikiana na kampuni ya GSM Foundation amesaidia waathirika wa tetemeko la ardhi wa mkoa wa Kagera kwa kukabidhi magodoro 400.
Jokate ambaye pia ni msanii wa luninga alikabidhi magodoro hayo kwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu, Salum Kijuu makoa makuu ya mkoa huo.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Jokate alisema kuwa kampuni ya GSM Foundation nay eye wameguswa na athari za tetemeke hilo ambalo mbali ya baadhi ya watu kupoteza maisha, kuna waathirikia mbalimbali.
Jokate alisema kuwa kuna watu wamepoteza makazi yao ya kuishi na mali zao mbalimbali, jambo ambalo limewafanya kurudi nyuma katika kimaisha.
Alisema kuwa magodoro ni moja ya mahitaji makubwa ya wahanga katika mkoa huo kuamua kukabidhi kontaina la futi 40 kwa Mkuu wa Mkoa.
“Ni janga la kitaifa kwani waliokumbwa na matatizo hayo ni watanzania wenzetu na wanahitaji msaada mkubwa, kuna majeruhi, kuna waliopoteza wazazi na jamaa zao huku wanafunzi wakikosa sehemu ya kusomea,” alisema Jokate.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu aliwashukuru Jokate na kampuni ya GSM Foundation kwa msaada huo ambao utapunguza changamoto za wahanga wa tetemeko hilo.
“Namshukuru Jokate na kampuni ya GSM Foundation kwa msaada huu, ni msaada mkubwa, lakini bado tunahitaji misaada zaidi, bado kuna changamoto nyingi sana kwa wahanga, hivyo tunaomba mashirika, watu binafsi na wadau wengine waunge mkono katika janga hili,” alisema Kijuu.
Alisema kuwa kama kila Mtanzania atachangia sh 100, wataweza kukusanya jumla ya Sh bilioni 5 ambazo zitawasaidia kuondoa changamoto mbalimbali na kuwafanya wahanga kurejea katika maisha yao ya kawaida.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (kushoto) akizungumza mara mara baada ya kupokea moja ya magodoro 400 yalitolewa na Kampuni ya GSM Foundation kupitia kwa Miss Tanzania namba 2 wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo (kulia).
No comments:
Post a Comment