Sunday, 18 September 2016

RAIS MAGUFULI APOKEA RIPOTI YA MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha cha  dola laki mbili za Kimarekani (USD 200,000) -takriban Tshs. 437,000,000/-  taslimu kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha ( wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia waathirika  wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa fedha  cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) - takriban Tshs. 437,000,000/- taslimu uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kusaidia waathirika watetemeko la ardhi mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani
Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma
taarifa kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Boniface Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais  Uhuru Kenyatta  wa Kenya na kwa misaada mbalimbali ya mabati 4,000 na vifaa vya majumbani ikiwemo magodoro na mashuka ambayo
inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka Kenya muda wowote kuanzia sasa. Katikati ni Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa fedha dola laki mbili za Kimarekani (takriban Tshs. 437,000,000/- )  taslimu kutoka Uganda pamoja na taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kutoka
kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment