Wednesday 14 December 2016

MAMBO MUHIMU ALIYOYAZUNGUMZA RAIS MAGUFULI JANA



'Nawaomba mtembee kifua mbele ninyi ndio watawala, hakuna chama kingine tawala'

'Zile nafasi za mwenyekiti kuchagua wajumbe wa NEC zimepungua, badala ya 10 nitachagua 7, lengo kutengeneza mwelekeo wa chama kipya'

'Tunaposema yaliyopita si ndwele tugange yajayo sio kwamba tumeyasahau yaliyopita, niwaombe tuendelee kukijenga chama

'Nimeshapata mialiko karibu ya 50 lakini nimeamua kusafisha nyumba yangu kwanza kabla ya kwenda kusafisha kwa jirani.

'Bei ya korosho imepanda kutoka 1000 hadi 4000 kwa kg 1 na walivyo wale watani zangu wameamua kuwanywesha mbuzi bia-

'Katika awamu hii hatutamsamehe mtu yeyote wa kutafuta uongozi kwa njia ya rushwa'

'Napongeza kamati za siasa za wilaya, mikoa ambazo zimechukua hatua dhidi ya waliotusaliti kwenye uchaguzi mwaka jana

'Wapo wanachama wachache ambao Hukisaliti chama chetu hasa kipindi cha uchaguzi na wengine kuendeleza makundi'

'Rasimali nyingi hatunufaiki nazo kutokana na mikataba isiyo na tija, usimamizi mbovu na ubadhirifu'-

'Tunataka chama chetu kijitegemee kiuchumi, ni aibu kutegemea fedha za ruzuku na watu binafsi ili kujiendesha'

'Tunataka kununua meli mbili, moja ziwa Tanganyika na nyingine ziwa Victoria'

'Napenda tuwe na chama kinachoongozwa na wanachama na sio chama kuongozwa na mtu chama ni mali ya wanachama'

'Nitapenda kuwa na jumuiya za chama zinazozingatia matakwa ya chama'-

'Nitapenda chama changu CCM kizingatie kanuni za uchaguzi ikwemo kanuni ya kiongozi kuwa na nafasi moja tu ya uongozi-

'Hatutaki kuwa na chama legelege cha watu walalamikaji, sisi ndio tumepewa ridhaa na wananchi kuongoza'-

'Hii haitakuwa mara ya mwisho tutakapoamua hakuna mtu atakayenipangia nifanyie mkutano wapi.

'Vyama vingine wakitaka kufanya vikao hapa Ikulu waombe ila tutataka kujua ajenda zao'

'Sioni aibu ya kuwakaribisha wanaCCM hapa Ikulu maana bila ninyi nisingefika hapa, hapa ni mahali pa watanzania wote'

No comments:

Post a Comment