WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amemtembelea na kumpa pole Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Steven Ngonyani (Profesa Majimarefu).
Mbunge huyo machachari, amelazwa katika Hospitali ya Kairuki, Mikocheni, Dar es Salaam, akipatiwa matibabu.
Akiwa hospitalini hapo jana, Waziri Mkuu alisema amefurahi baada ya kumkuta mbunge huyo akiwa anaendelea vizuri na kwamba afya yake inaridhisha.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumtakia afya njema Majimarefu na kusema anaamini hivi karibuni atapona na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kwa upande wake, mbunge huyo alimshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kumjulia hali.
Pia, alisema anamshukuru Mungu kwamba anaendelea vizuri na anatarajia kwenda nchini India, kwa matibabu zaidi baada ya utaratibu kukamilika.
No comments:
Post a Comment