Sunday 23 July 2017

MWANAMKE MTANZANIA AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA INDIA


Mwanamke Mtanzania amekamatwa na Polisi wa Samrala, India, akiwa na dawa za kulevya aina ya heroine gramu 300, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mwanamke Mtanzania kukamatwa akiwa na dawa hizo kwenye jimbo hilo.

Katika taarifa iliyochapishwa na mtandao wa The Tribune wa India, Mtanzania huyo, ambaye ni mwanamitindo anayefanya kazi zake Delhi na Mumbai, alikamatwa na polisi waliokuwa kwenye doria katika eneo liitwalo ITI-Samrala.

Baada ya kukamatwa, alikutwa ameshikilia paketi ya biskuti na baada ya kuwaona polisi, alianza kula biskuti hizo, lakini walipomfikia na kufungua paketi, waligundua ni dawa za kulevya aina ya heroine.

Katika uchunguzi wa awali, mwanamke huyo alieleza kuwa alisafiri kutoka Delhi kuuza dawa hizo kwa mtu aliyeishi Ludhiana. Tayari amefunguliwa mashtaka na atafikishwa Mahakamani.

No comments:

Post a Comment