Sunday, 20 September 2015

LIPUMBA NA SLAA VIDUME- MAKAMBA


NA THEODOS MGOMBA, MTERA

KATIBU Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, amesema wanamume wa kweli ndani ya upinzani ni wawili ambao wamekataa uozo na kujitoa katika vyama vyao.

Makamba aliwataja wanamume hao kuwa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa.

Alisema hayo juzi wakati akizindua kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde, zilizofanyika katika Kata ya Mpwayungu.

Makamba alisema viongozi hao wawili wameonyesha uzalendo na kukerwa na ufisadi.
na kuwa baada ya kuona CHADEMA wanaingia mafisadi, wao walijitoa na hawakumung’unya maneno.

Alisema kiongozi anayegombea nafasi ya urais kupitia CHADEMA si muadilifu na kama atabisha ajibu hoja alizomuuliza alipokuwa Morogoro ili atoe tena zingine.

‘’Hawa kati ya wanamume wa kweli ni wanamume kwani mara baada ya kuona fisadi anaingia katika UKAWA wao waliondoka kwani dhamira ziliwasuta, hao wengine ni mafisadi kama walioingia hivi karibuni," alisema Makamba.

Na kama CHADEMA ni chama chenye watu makini wasingekuja kuchukua fisadi ambaye CCM imemkata jina hiyo ni dalili kuwa hawana watu wa kuwaongoza,’’ alisema.

Alisema ni lazima mtu anapotaka kuchagua chama anatakiwa kuhakikisha kuwa watu wa chama husika ni makini na wana uwezo wa kuwaoongoza wengine bila kigugumizi.

Katibu huyo alisema viongozi wa CCM wote waliopita na wanaoomba kupata ridhaa ya kuwa viongozi wana historia ndani na nje ya nchi.

‘’ Hata ukiangalia safu ya viongozi hao utaona kuwa ni watu makini ukianzia Nyerere (Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli, sasa huyo Mbowe ana historia gani ndani ya nchi hii?’’ alisema Makamba.

No comments:

Post a Comment