Monday 28 September 2015

LOWASSA ASHINDWA KUHUTUBIA WANANCHI TANGA, ADAI HALI YAKE SI NZURI




Mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa, jana alishindwa kuwahutubia wananchi wa Tanga kuwaomba kura, licha ya kutakiwa kuzungumza kwa dakika tano.
Badala yake, Lowassa aliwaeleza wananchi hao kuwa, ifikapo Oktoba 25, mwaka huu, wajitokeze kumpigia kura na kwamba, hataweza kuzungumza kutokana na hali yake aliyokuwa nayo bila kufafanua zaidi.
Hata hivyo, kabla ya Lowassa kukaribishwa kupanda jukwaani na kuzungumza maneno mawili, Tambwe Hizza, alikiri kuwa mji wa Tanga umepiga maendeleo makubwa.
Pia, Tambwe ambaye amehamia UKAWA, alikuwa kwenye wakati mgumu pale alipojikuta akimnadi aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, akiwaomba wananchi wampe kura badala ya kumuombea Lowassa.
Hayo yalijiri jana katika Uwanja wa Tangamano jjini hapa, ambapo wananchi waliojitokeza kuwasikiliza viongozi hao walipigwa na butwaa.
Hata hivyo, Tambwe aliwaomba radhi wananchi hao na kudai kuwa amejikuta akimnadi Profesa Lipumba kutokana na kuwa naye karibu.

No comments:

Post a Comment