Sunday, 20 September 2015

LUSINDE AWASHUKIA WANAHABARI


KATIKA  hali isiyo ya kawaida Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Jimbo la Mtera amewashukia waandishi wa habari na kuwataka wawe wakweli katika kazi zao vinginevyo rushwa itawamaliza.

Mbunge huyo Livingstone Lusinde aliyasema hayo juzi wakati akiongea na wakazi wa jimbo hilo mara baada ya kuzinduliwa kwa Kampeni za Chama katika Jimbo hilo.

Alisema inashangaza kuona kuwa mgombea nafasi ya urais kupitia CHADEMA Edward Lowasa amekuwa akiandikwa kwa kirefu katika baadhi ya magazeti huku mgombea huyo huwa anaongea kwa dakika mbili au tatu tu.

‘’ Mtu akifika katika mkutano anazungumza kwa dakika mbili au tatu lakini nyie ndugu zangu kesho ukisoma katika magazeti unakuta kurasa nzima au mbili haya mengine mnayatoa wapi acheni rushwa itatuumiza jamani’’ alisema Kibajaji.

Alisema kwenye masuala yanayohusu maslahi ya taifa hatutakiwi kuzungumzia mtu bali uwezo wake kwani anakwenda kuwatumikia watu na si mtu’’

‘’ Nawaoomba viongozi wa dini watuombee nchi yetu ifanye uchaguzi huu kwa amani na utulivu ili tusonge mbele,’’ alisema.
 
Aidha mgombea ubunge huyo alimuomba mgombea huyo wa CHADEMA kuwa na mdahalo wa mgombea wa urais wa CCM ili kuona ubora, uwezo na umakini kati ya watu hao wawili.

‘’ Tunataka kuwepo kwa mdahalo wa wagombea hao hata kama ni wa saa tano tu wote wasimame tuone kama nani ataweza, rais ni lazima awe mzima kiafya na kiakili’’ alisisitiza.

Alisema yeye binafsi ana uhakika kuwa mgombea huyo katika jimbo hilo kuna vituo atapata kura sifuri kwani wana CCM wamejipanga kuhakikisha hilo linafanyika.

Lusinde aliwataka wagombea wengine wote ambao hawakuweza kupata nafasi katika kugombea udiwani wajiunge pamoja na kusahahu tofauti zao wakati wa kugombea kura za maoni kwani sasa ni kitu kimoja na kazi iliyo mbele yao ni kuhakikisha CCM inashinda.

‘’Nawaoomba mpigieni kura za ndiyo ili aweze kushika Dola akiwa na madiwani wote wa CCM na siyo kuchanganya changanya kwani kuna madhara yake’’ alisema Lusinde.

Akizungumza katika mkutano huyo mgombea ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Felister Bura aliwatadharisha wakazi wa mkoa huo wakiwemo wakina mama na vijana kuwa macho na kadi zao za kujiandikisha kupiga kura .

Alisema hivi sasa kuna baadhi ya watu wanapita na kununua kadi hizo kwa madai ya kwenda kuhakiki na hapo uturoka navyo.

Alisema kwa upande wa vijana watu hao wamekuwa wakiwadanganya kuwa wanachukua kadi hizo ili kwenda kujua kama ni raia wa Tanzania waweze kuwapatia ajira jambo ambalo si kweli.

Kwa mujibu wa Felister alisema baada ya kuchukua kadi hizo huzipiga ‘’Fotocopy’’ na kisha kuwaachia vijana hao kopy hizo na kuondoka na vitambulisho halisi.

"Mkumbuke kuwa mkifanya hivyo hamtapiga kura siku ikifika kwani hivyo ndivyo vitakavyohusika katika kuhakikiwa kabla ya kupiga kura’’ alisema.

Katika hatua nyingine, Makamba aliwaoomba wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha kuwa wanamchagua Livingstone Lusinde kwani pamoja na kuitwa kibajaji wakati uliopita sasa amekua na kustahili kuitwa burdozeer.

Naye kibabaji akiomba kura za wakazi wa Jimbo hilo alisema ni muhimu wakachagua Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kukamilisha kazi mbalimbali walizozianza.

Alisema hivi sasa tayari wameshawailisha ombi la kuigawa Wilaya ya Chamwino ili kuweza kuwafikishia wananchi huduma muhimu.

Alisema kazi hiyo itakamilika tu endapo CCM itaongoza Jimbo hilo kwani ndiyo chama kilichoanzisha mchakato huo

No comments:

Post a Comment