Na
Clarence Chilumba, Masasi
ASKOFU
wa Kanisa la Sayuni International Pentekoste, Masasi mkoani Mtwara, Angelus
Mchomanjoma, amewataka Watanzania kuilinda amani iliyopo ambayo ni tunu kwa
taifa.
Alitoa
wito huo jana wakati akizungumza na Uhuru kuhusu maandalizi ya tamasha la
kuombea amani mkoa wa Mtwara, litakalofanyika keshokutwa kwenye viwanja vya
Boma mjini Masasi.
Alisema
lengo la tamasha hilo ni kuombea amani ili matokeo ya uvunjifu wa amani
yasijitokeze kipindi hiki cha kampeni na baada ya matokeo kutangazwa na kwamba rais
atakayechaguliwa ndiye chaguo la Mungu.
Mchomanjoma
alisema tamasha hilo la kuombea amani mkoani Mtwara litashirikisha
maaskofu,wachungaji pamoja na waimbaji kutoka kwenye kwaya mbalimbali za
makanisa ya Kipentekoste kutoka ndani na nje ya mkoa huo.
Alisema
tamasha hilo lenye lenye kauli mbiu ya ‘Umoja wetu ndio msingi wa amani yetu’,
ni sehemu muafaka kwa maaskofu na wachungaji wa umoja wa makanisa hayo,
kuhubiri neno la Mungu kwa ajili ya kulinda na kuitetea amani kipindi chote cha
uchaguzi.
No comments:
Post a Comment