Msafara wa mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli ukiingia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha |
Umati wa wananchi uliofurika kwenye mkutano wa kampeni wa Dk. Magufuli mjini Arusha |
Dk. Magufuli akiwahutubia wananchi mjini Arusha |
Dk. Magufuli akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo |
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wakati wa mkutano huo |
Dk. Magufuli akishangiliwa na wananchi wakati msafara wake ulipokuwa ukiingia uwanjani |
Mgombea ubunge wa jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka akihutubia wananchi |
Dk. Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Monduli, Namelok Sokoine |
Dk. Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu wa zamano, Edward Moringe Sokoine |
NA CHARLES MGANGA, ARUSHA
MGOMBEA urais wa CCM, Dk. John Magufuli, amewahakikishia Watanzania kuwa uongozi wake utafuata nyayo za Hayati Moringe Sokoine.
Amesema maslahi
ya Watanzania, hasa wanyonge yatazingatiwa na kwamba hakutakuwa na nafasi kwa
viongozi na watendaji wala rushwa.
Pia ameelezea kushangazwa na umati mkubwa uliojitokeza
katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini hapa na kufananisha hali hiyo na
mafuriko ya tsunami.
Amesema umati huo umemfurahisha na kudhihirisha ukweli kwamba, tayari Watanzania wameshakubali yeye ndiye rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
“Hakika Arusha mmefunika. Idadi kubwa ya watu kiasi hiki, hii haijapata kutokea… ni funga kazi kweli kweli.Mmenifurahisha sana.
“Kuna waliosema Arusha sitapata watu, wote hawa kila kona kweli, Watanzania wameamua kutaka mabadiliko na tayari nimeshashinda,” alisema Dk. Magufuli.
Amesema umati huo umemfurahisha na kudhihirisha ukweli kwamba, tayari Watanzania wameshakubali yeye ndiye rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
“Hakika Arusha mmefunika. Idadi kubwa ya watu kiasi hiki, hii haijapata kutokea… ni funga kazi kweli kweli.Mmenifurahisha sana.
“Kuna waliosema Arusha sitapata watu, wote hawa kila kona kweli, Watanzania wameamua kutaka mabadiliko na tayari nimeshashinda,” alisema Dk. Magufuli.
Aidha, Dk. Magufuli ambaye awali alifanya mikutano katika maeneo ya Mto wa Mbu, Monduli na Longido, aliwashukia watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuwataka kujiandaa kuondoka katika nafasi zao kutokana na tatizo la kukatika umeme kila wakati.
Alisema haiwezekani, umeme ukatike katika kipindi cha
kampeni, huku akisema wanaodhani, wanafanya hivyo kwa ajili ya kumkomoa
wanajidanganya.
Pia, alisema mawaziri wanaoshughulika na umeme
wanapaswa kuajiangalia kwani, kukatika kwa umeme mara kwa mara kunasababisha
umasikini kwa Watanzania.
“Haiwezekani kabisa umeme uwe unakatika kipindi hiki
cha kampeni. Tatizo hili limeongezeka kwa kiasi kikubwa. Wanataka Watanzania
wanichukie ama waichukie CCM… watu wa umeme wajiandae,” alisema huku
akishangiliwa na umati wa watu.
Alisema kukatika kwa umeme kunaweza kuwa kunafanyika
kwa sababu zisizo na msingi na zilizoegemea katika itikadi za kisiasa.
Hata hivyo, aliwataka Watanzania kuvumilia, kwani zimesalia
siku 17 tu kabla ya uchaguzi, ambapo akichaguliwa atachukua hatua kali dhidi ya
vitendo vya ukataji wa umeme wa hovyo.
Akizungumzia suala la ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Dk. Magufuli alisema serikali yake itaendelea kuimarisha uhusiano na
nchi zinazoizunguka Tanzania.
Alisema kwa kufanya hivyo, kutaendelea kuwezesha mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia ambayo tayari umeshajengwa na awamu za serikali, zilizotangulia.
“Nitaendelea kuimarisha uhusiano wetu mzuri na nchi za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na zingine zilizo karibu.
“Kenya ni majirani zetu, tutaendeleza ushirikiano wetu wa kibiashara kama ilivyo sasa,” alisema Magufuli.
Pia, Dk. Magufuli aliwaambia watu waliobinafsishiwa
viwanda, kuviendeleza kabla ya siku ya kuingia madarakani.
Alisema kitendo cha viwanda hivyo kutoendelezwa, kinawakosesha vijana ajira na kuinyima serikali mapato.
Alivitaja baadhi ya viwanda hivyo ni kile cha matairi
cha General Tyre, ambacho kilisaidia vijana wengi kufanya kazi hapo.
na kiwanda cha nguo cha Kiltex, ambavyo amevitaka vianze kazi mara atakapoingia madarakani.
na kiwanda cha nguo cha Kiltex, ambavyo amevitaka vianze kazi mara atakapoingia madarakani.
“Nimeshasema na narudia, waliobinafsishiwa viwanda na
wameshindwa kuviendeleza wajiandae kuvirejesha ama kuviendeleza,” alisema.
Alisema wakishindwa kuviendeleza viwanda hivyo,
atavirejesha serikalini kwa manufaa ya Watanzania wote.
Mgombea huyo wa CCM, alisema serikali yake inataka
kujenga Tanzania mpya ya viwanda. Itajenga viwanda vikubwa vya kati na vidogo,
kwa ajili ya kuwawezesha vijana kujiajiri na kuajiriwa.
Alisema serikali yake inataka kufanya mabadiliko
makubwa, hivyo amewataka wale wanaobeza, kuwapuuzwa.
Dk. Magufuli alisema anachoamini maendeleo hayana chama,
udini, wala ukanda, jambo la msingi ni kuungana kufanikisha ndoto hiyo ya
kuijenga Tanzania mpya.
“Nimekuwa nikisema, maendeleo hayana chama, dini wala
ukanda. Jambo la msingi, tuungane kwa pamoja, tushirikiane na kushikamana kuyapata
maendeleo,” aliongeza.
Dk. Magufuli alisisitiza kwamba wawekezaji kuzingatia
masharti ya kuajiri Watanzania kwa asilimia fulani kinyume na wanavyofanya
wawekezaji wengi kwa kuja na wafanyakazi wao.
Kuhusu utalii alisema ana mpango wa kuibadilisha Arusha, iwe kitovu cha utalii katika ukanda wa Afrika.
Alisema anashangazwa na umaarufu wa Arusha kutoweka,
hivyo serikali yake inakusudia kurejesha hadhi hiyo iliyotoweka kwa muda mrefu
sasa.
“Arusha ni mji wa utalii, lakini hadhi hiyo imetoweka
kabisa kwa sababu zisizoeleweka, serikali yangu nitakayoiunda kuujenga upya mji
wa Arusha uweze kuendelea kukuza sekta ya utalii wetu,” alisema Magufuli.
Dk. Magufuli alisema atahakikisha tatizo la maandamo
ambalo lilikuwepo na kufanywa na watu wa upinzani mpaka kupoteza, amani kwa
watalii, hali hiyo itarekebishwa na serikali yake.
“Maandamano yaliyokuwa yakifanyika mjini Arusha,
yamekuwa yakiwaletea hofu watalii na hivyo kupunguza idadi ya watalii nchini.
Serikali yangu italishughulikia hilo,” alisema.
Alisema si hayo tu, serikali atakayoiunda, imedhamiria kufanya mambo makubwa, jambo la msingi ni kurejesha amani na hadhi ya Arusha iliyopotea.
Dk. Magufuli aliwahakikishia watu waliovunjiwa nyumba
zao kupisha ujenzi wa barabara jijini Arusha kuwa zimetengwa sh. bilioni 22 kwa ajili ya kuwalipa kwa
mujibu wa sheria.
“Hawa wala wasiwe na wasiwasi, fedha zimeshatengwa kwa
ajili ya kuwalipa haki yao kwa mujibu wa sheria ya ardhi na ile ya mipango miji
namba 4 na 5 ya mwaka 1999,” alisema Dk. Magufuli.
KUFUATA NYAYO ZA SOKOINE
Dk. Magufuli alisema
anataka kufanya kazi kwa kufuata nyayo za Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Moringe
Sokoine.
Alisema marehemu Sokoine
alikuwa akipiga vita ufisadi, rushwa na uzembe na kwamba atahakikisha serikali
yake itatatua matatizo ya Monduli.
Dk. Magufuli, ambaye kabla
ya kuzungumza na wananchi wa Monduli, alizuru kaburi la Sokoine, alisema
atahakikisha mabwawa ambayo yaliyobomoka, yanatengenezwa, ili kupunguza kero ya
maji na maeneo ya kunyweshea mifugo.
"Sipendi mafisadi na
siku zote nimekuwa mkweli kusimamia hilo... hata Sokoine alichukia hayo pamoja
na watu kuonewa, nitafuata nyayo zake. Nitatengeneza haya kumuenzi Hayati
Sokoine," alisema Dk. Magufuli.
Aidha alisema kwamba serikali yake itahakikisha hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa. Pia alitumia fursa hiyo kuwatoa hofu wananchi wanaotishwa kuwa siku ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani na kusema ulinzi utaimarishwa, ili kila Mtanzania atimize haki yake ya kikatiba.
"Nasikia mnatishwa na
baadhi ya watu…tunajua huo ni mkakati ili kuvuruga uchaguzi…jitokezeni kwa
wingi na mkadhihirishe kwa kuipigia kura nyingi wagombea wa CCM," alisema
Dk. Magufuli.
Aliongeza kusema ana uhakika hata kama kura zikipigwa leo, ataibuka mshindi katika nafasi anayogombea.
Alisema anajua wapinzani
wamekuwa wakitoa fedha kwa wananchi, hivyo aliwataka wachukue, lakini wachague
viongozi wa CCM.
"Hizo fedha chukueni, kuleni kwa sababu ni zenu, mafisadi waliwaibieni siku nyingi," alisema Dk. Magufuli.
KINANA: VIKAO VIFUTWE
Wakati akizungumza, Kinana aliishauri serikali ya Dk. Magufuli
kufuta vikao vya watendaji, kwani vinachangia kukwamisha ufanisi na kuwahudumia
watu kwa wakati.
Kinana alisema vikao hivyo ni vyema vikapunguzwa au kufutwa kabisa kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi katika kuongeza kasi ya maendeleo.
Dk. Magufuli ambaye tayari ameshafanya mikutano ya
kampeni mikoa 21, ataendelea kuomba kura maeneo mengine ya jiji la Arusha,
kabla ya kuingia Mkoa wa Kilimanjaro.
HUJUMA ZA UKAWA ZAKWAMA
Hujuma na mchezo mchafu
uliopangwa na viongozi na wafuasi wa UKAWA dhidi ya mikutano ya Dk. Magufuli
jana, zilishindwa kupambana na nguvu na hamasa ya wananchi.
Awali, viongozi wa UKAWA
mkoani hapa walitekeleza maelekezo ya wakubwa wao kwa kuandaa vijana wa kumzomea
Dk. Magufuli na msafara wake pamoja na kutangaza hali ya hatari ili kuwazuia
wananchi wasihudhurie mkutano huo.
Pia, walikodisha vyumba
kwenye hoteli nyingi jijini hapa kuzuia msafara huo usipate malazi pamoja na
kutangaza kuwa mikutano ya Dk. Magufuli na wagombea wa CCM imefutwa.
Hata hivyo, mchezo mchafu
huo ulibainika mapema na kudhibitiwa na mambo kwenda kama yalivyopangwa.
BENKI MTO WA MBU
Akiwa eneo la Mto wa Mbu,
Dk. Magufuli alisema atahakikisha Benki ya CRDB inafungua tawi, ili
wananchi wapate huduma za kifedha.
Alieleza masikitiko yake
kwa viongozi waliokuwa wakiongoza Jimbo la Monduli kushindwa kuzungumza na
benki ili kufungua matawi ya kuwahudumia wananchi.
Pia alimwomba Meneja wa
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kufungua ofisi katika eneo hilo, kwa ajili
ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
"Nitaongea na viongozi
wa taasisi na mamlaka husika kuangalia uwezekano wa kufungua tawi kwa ajili ya
huduma kwa wananchi,” alisema.
Aliwaomba wananchi
kumchagua mgombea ubunge wa Monduli, Namelok Sokoine, ili awaletee maendeleo ya
haraka.
Alisema Namelok ataendeleza
yale ambayo Hayati Sokoine, aliyodhamiria kuyafanya enzi ya uhai wake.
Akiwa, Longido, Dk. Magufuli
aliahidi serikali yake kutatua changamoto zilizopo ndani ya wilaya na jimbo
hilo.
Moja kati ya ahadi hizo ni
kuanzisha soko la mifugo, ambalo litainua kipato chao na kuahidi kuwa serikali yake itakuwa karibu na wafugaji
kwa kuwapa elimu na kuwawezesha kukopa.
Suala la mpango wa matumizi bora ya ardhi, nalo alisema litazingatiwa katika kipindi cha awamu ya tano ya serikali yake.
"Nitaimarisha mfuko wa maendeleo ya mifugo, ili wafugaji wafanye ufugaji wenye tija," alisema Dk. Magufuli.
Kabla ya Dk. Magufuli
kupanda jukwaani, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, aliwasalimia wananchi
na kusema wale wenye mashaka na CCM, wanapoteza muda.
"Tayari ushindi ni wa
Magufuli kwa sababu atatua kero za Watanzania," alisema Kinana.
Aliwaambia wananchi wa Longido kwamba Dk. Magufuli ni mwadilifu na mchapakazi hodari.
No comments:
Post a Comment