Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akitia saini kitabu baada ya kuripoti ofisini kwake jana |
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal na baadhi ya wafanyakazi wa ofisi yake jana |
NA MWANDISHI WETU
MAKAMU wa Rais,
Samia Suluhu Hassan, amewataka watumishi wa ofisi yake kufanyakazi kwa bidii na
kwamba watakaopitwa na kauli mbiu ya ‘Hapa kazi tu’, wakae pembeni.
Samia alisema hayo
jana, Ikulu mjini Dar es Salaam, baada ya kukabidhiwa ofisi na Makamu wa Rais mstaafu,
Dk. Mohammed Gharib Bilal.
Baada ya
makabidhiano hayo, Samia alikaribishwa na watumishi wa ofisi yake, ambapo
alitumia fursa hiyo kuwataka kufanyakazi kwa bidii kulingana na kauli mbiu ya
'Hapa ni kazi tu'.
“Kila mmoja afanyekazi
kwa bidii mahala pake pa kazi. Wale ambao kauli mbiu ya Hapa ni kazi tu
itawapita, wakae pembeni, watatusamehe,” alisema Samia akiwaonya watumishi hao.
Aliwataka watumishi
wa ofisi hiyo kupendana na kushirikiana ili kufanikisha azma ya kuleta
matarajio ya maendeleo ya Watanzania, wanayotaka kuyaona katika uongozi wa
awamu ya tano.
Makamu huyo wa rais,
baada ya kutoa nasaha hizo, alifanya kikao na menejimenti ya ofisi, ambapo
alitoa uelekeo wa utendaji kazi katika ofisi hiyo, hususan kuzingatia kusimamia
masuala ya muungano na mazingira ili kufanikisha malengo ya serikali.
Samia aliitaka menejimenti
hiyo kujipanga upya na kuacha kufanyakazi kwa mazoea kwa ajili ya kuleta
mabadiliko kwa upande wa masuala ya muungano na mazingira.
No comments:
Post a Comment