Na Mwandishi Wetu
MSAJILI wa Vyama vya
Siasa, Jaji Francis Mutungi, ametoa cheti cha usajili wa muda kwa Chama cha
Tanzania Patriotic Front (TPF Mashujaa).
PTF-Mashujaa ni chama cha 23, katika
orodha ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa nchini, tangu kuanza kwa mfumo wa
vyama vingi mwaka 1992.
Akizungumza na waandishi wa habari, jana, Dar es Salaam, Jaji Mutungi alisema cheti hicho kwa mujibu wa sheria ni cha siku 180, ambapo chama hicho kitatakiwa kutafuta wanachama 200, katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na miwili ya Zanzibar.

Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho,
Deonatus Mutani alisema lengo lake
ni kulinda, kutetea na kudumisha uhuru, haki, amani na ustawi wa nchi na raia
wote.
"Malengo mengine ni kupambana
kisiasa ili kulinda fedha, rasilimali za nchi na urithi wa asili wa nchi visiporwe,
visidhudumiwe au kitumiwa vibaya na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa
dhidi ya kikundi chochote cha watu kitakachopanga kuiba, kuhamisha, kuhujumu,
kutumia vibaya fedha na rasilimali za nchi," alisema.
Alisema walifanya utafiti kwa muda
mrefu na kuzingatia hali ya kisiasa na
vyama vilivyopo na kubaini kuwa, hakuna mahitaji mengi ya kisiasa yanayohitaji
majibu kwa kupitia chama cha siasa kilichojipanga vyema.
"Tunahitaji chama kinachowatumikia na kumilikiwa na wananchi badala ya wananchi kukitumikia chama na kitakachowakwamua wananchi katika mfumo, ambao siasa inachukuliwa kama jambo la mpito, hasa wakati wa uchaguzi na mijadala bungeni," alisema Mutani.

Aliongeza kuwa wamepitia katiba za vyama mbalimbali na kuona mapungufu
ambayo hayawezi kushabiliana na ushujaa wanaotaka kujenga katika vyama vyote, mwanachama
anayekosoa sera za chama hadharani na kutofautiana na misimamo ya viongozi
wenzake.
Mutani alisema wameheshimu na kuruhusu demokrasia ya kweli ndani ya chama, viongozi wakuu wa chama na wale wanaogombea nafasi za uongozi katika dora watajadiliwa katika matawi na kutoa tamko huru la madai.

"Binadamu wote wanastahili kuheshimiwa, kuthaminiwa, kutendewa haki,
kumiliki mali binafsi na kushiriki kataka maendeleo ya nchi bila kijali tofauti
zilizopo miongoni mwao, ndio maana tumeamua kuanzisha chama cha kawaida, kwa
ajili ya watu wa kawaida na maisha ya kila siku kwani siasa ni
maisha," alisema Mutani.
Alisema chama hicho hakina udini
wala ukabila, isipokuwa kazi yake kubwa ni kutangaza sera za chama hicho kwa
maendeleo ya jamii.
No comments:
Post a Comment