Tuesday, 24 November 2015

WABUNGE WAGONGA MWAMBA KWA MAGUFULI


NA MWANDISHI WETU, DODOMA

SERIKALI ya Rais Dk. John Magufuli imeendelea na mikakati yake ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili fedha nyingi kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo huduma za kijamii.

Tayari ameanza kutekeleza azma yake hiyo kwa kusitisha safari za nje kwa viongozi wa juu wa serikali, ambapo safari hii shughuli imehamia bungeni.

Habari za kuaminina zinasema kuwa, serikali imegoma kuongeza posho na mishahara kwa wabunge, ikiwa ni pamoja na nyongeza ya fedha za mkopo wa magari.

Habari kutoka kwenye chanzo chetu zimesema kuwa, wabunge wataendeleakukopeshwa sh. milioni 90 kwa ajili ya kununua magari ili kuwarahisishia kutekeleza majukumu yao kwenye majimbo.

Kwa mujibu wa utaratibu, wabunge wanatakiwa kununua magari aina ya ‘Hardtop’. Pia wameelezwa kuwa wataendelea kupokea posho ya sh. 300,000 kwa siku.

Hata hivyo, habari zinaeleza kuwa uamuzi huo wa serikali haujawaridhisha wabunge wengi na kumwomba Katibu wa Bunge kushughulikia suala hilo.

“Hardtop zenyewe hivi sasa bei ya soko ni zaidi ya sh. milioni 130, sasa hiyo sh. milioni 90, tutaifanyia nini?” Alihoji mbunge mmoja, ambaye hakutaka jina  lake litajwe gazetini.

Imeelezwa kuwa baada ya kikao cha wabunge na viongozi wa utawala bungeni, wengi walionekana kutoridhika na kumwomba katibu afuatilie suala hilo.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge walipongeza hatua hiyo ya serikali na kusema kuwa, uzoefu unaonyesha kuwa sio wote wanaonunua magari yanayoweza kuhimili barabara za vijijini.

“Kuna wengine wanatumia RAV 4 hapa, sasa hizo milioni 130 za nini? Hata hizo 90 ni nyingi,” alisema mbunge mmoja.

Wakati wabunge wananung’unika na kutaka pesa zaidi, imebainika kuwa ofisi ya bunge ni miongoni kwa vyombo vyenye matumizi makubwa, ikiwemo safari za nje.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa walipongeza msimamo wa serikali na kutaka kutowasikiliza, kwani wengi wamekuwa wabinafsi.

Bakari Mtendewa, mkazi ya Dodoma, alisema tatizo baadhi ya wabunge wamekuwa na maslahi binafsi, badala ya maendeleo ya wananchi majimboni.

Alisema wabunge wamekuwa wakidai maslahi yao binafsi, badala ya wananchi, hivyo wakati wa mabadiliko wa kuacha kuchezea pesa za serikali ni sasa.

Wakati uamuzi huo unafikiwa, tayari Rais John Magufuli ameshatoa maelekezo kwa taasisi za umma kuacha matumizi mabaya ya fedha, badala yake fedha hizo zitumike katika huduma muhimu kama vile, afya na elimu.

Mwishoni mwa wiki, Dk. Magufuli alizuia matumizi ya sh. milioni 250 za bunge, zilizochangwa na wadau kwa ajili ya mchapalo na kuagiza fedha hizo zitumike kwa kununulia vitanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Alielekeza kutumika sh. milioni 15 na isizidi sh. milioni 20. Sherehe hiyo ilikuwa ni tofauti na katika vikao vya bunge vilivyopita, ambapo wabunge na wageni waalikwa hujumuika katika chakula cha usiku, kinachoambatana na vinywaji vikali na mvinyo, ambapo kwenye sherehe hiyo vinywaji laini vilitawala. Pia, wabunge waliburudishwa kwa muziki

No comments:

Post a Comment