NA MUSSA YUSUPH
KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo,Zitto Kabwe,amewashangaa wanasiasa wanaompinga Rais Dk. John Magufuli, akisema wana maslahi binafsi na mafisadi nchini.
AmesemaDk.Magufuli amedhamiria kwa dhati kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa vikilalamikiwa na Watanzania kwa kuwa ni adui wa haki.
Zitto (pichani) amesema nchi imempatakiongozialiyeamua kupambana na ufisadi, hivyo atashirikiana naye kwenye vita hivyo kwa sababu ACT inamtambua Rais Magufuli kama mshindi halali wa kiti hicho.
Kauli hiyo ya Zitto imekuja baada ya Rais Dk. Magufuli kulihutubia Bunge na kuonyesha kuchukizwa na vitendo vya rushwa na ufisadi. Katika hotuba hiyo aliyoitoa Alhamisi, wiki iliyopita, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Bunge la 11, Dk. Magufuli alisema vitendo vya rushwa na ufisadi vinawanyima haki wananchi na kuitia serikali hasara ya mamilioni ya fedha, ambazo zingetumika kwenye miradi ya maendeleo.
Alisemakwa Mtanzania mwaminifu, kwa imani yake hatakuwa na kigugumizi katika kuwa mstari wa mbele kupambana na rushwa pamoja na ufisadi.
“Mimi nimewaahidi wananchi na ninataka kurejea ahadi yangu mbele ya Bunge, kwamba nitapambana na rushwa na ufisadi bila kigugumizi na bila haya yeyote.
“Dawa ya jipu ni kulitumbua na mimi nimejipa kazi ya kuwa mtumbua jipu. Najua kutumbua jipu kuna maumivu, lakini halina dawa nyingine, hivyo nawaomba Watanzania waniombee,”alisisitiza Rais Dk. Magufuli.
Wakati Rais Magufuli akitoa hotuba hiyo iliyowasisimua wananchi kwa kutoa taswira ya dhati katika kukabiliana na ubadhirifu wa mali za umma, wabunge wa kambi ya upinzani kutoka kundi la UKAWA waliondoka bungeni.
Kabla ya Rais Dk. Magufuli kuanza kuhutubia, wabunge hao walianza kupiga kelele pasipo kuzingatia kile kilichowafanya kuchaguliwa na wananchi katika kujadili na kutatua matatizo ya wapigakura wao.
Licha ya wabunge wa UKAWA kutoka, Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo, alibaki bungeni kusikiliza hotuba ya rais. Kitendo hicho kilielezewa na chama chake kuwa ni msimamo wa kuunga mkono serikali ya Rais Dk. Magufuli na kwamba tafsiri ya uzalendo ni kumuunga mkono rais kukabiliana na watu walioligeuza taifa kuwa shamba la bibi.
Zitto alisema ACT itaendelea kushirikiana na serikali kwenye masuala yenye kushabihiana, hususan vita dhidi ya ubadhirifu.
Mwanasiasa huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa ‘Twitter’, alisema alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati za Bunge, alitoa taarifa mbalimbali dhidi ya wizi na uporaji uliofanywa kwenye zoezi la ubinafsishaji.
Mwanasiasa huyo amekuwa akikabiliwa na upinzani kutoka vyama vinavyounda UKAWA, kwa madai ya kumfananisha na msaliti kwa kutokutoka bungeni.
Zitto alisisitiza kuwa, kuwaita watu pindi mnapotofautiana mitazamo kwamba ni wasaliti, ni kielelezo kamili cha ujinga wa kisiasa.
Kwa upande wake, wakili maarufu nchini, Albert Msando kupitia ukurasa wake wa ‘Twitter’, alisema wakati Dk. Wilbroad Slaa alipompinga Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2010, alionekana shujaa.
Aliongeza kuwa, lakini mwaka huu, Dk. Slaa alipompinga aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, alionekana msaliti, hivyo alifananisha usaliti na kitendo cha kupinga maelekezo.
Wakati UKAWA wakisusia hotuba hiyo, wabunge hao jioni kwenye tafrija iliyofanyika Bungeni, ambako pia Rais Dk. Magufuli alihudhuria na kuzungumza, walionekana wakiwa kwenye foleni ya chakula kama kawaida yao.
Kitendo hicho kiliwashangaza wananchi na wabunge waliohudhuria tafrija hiyo, kwa kuhoji ingekuwa vyema UKAWA pia wangesusia.
Wakizungumzia hotuba hiyo ya Rais Dk. Magufuli, wabunge na wachambuzi wa masuala ya kisiasa walisema imeleta matumaini mpya kwa Watanzania.
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, alisema hotuba hiyo ni ya kihistoria na imetoa dira ya maendeleo kwa wananchi.
Alisema Rais Dk. Magufuli ameonyesha namna ambavyo dhamira yake ni ya kuwatumikia wananchi kwa kuchapakazi na kupambana na ubadhirifu.
Aliongezakuwaserikali atakayoiunda itafanyakazi karibu na wananchi katika kuwawezesha kiuchumi, hivyo wanasiasa na wananchi wanapaswa kuiunga mkono.
Naye mbunge wa Viti Maalumu kutoka mkoa wa Singida, Martha Mlata, alisema hotuba hiyo imetoa dira kwa kina mama, hususan kwenye uwezeshaji wa kiuchumi.
Pia alimpongeza Rais Dk. Magufuli kutilia msisitizo suala la ajira kwa vijana, ambapo alipongeza jitihada za serikali ya awamu ya tano za kufufua viwanda, ambavyo vitatoa ajira kwa vijana wengi kwenye kada mbalimbali za kielimu.
Kwa upande wake, Aysharose Mattembe (Viti Maalumu), alisema serikali ya Rais Dk. Magufuli imeonyesha namna itakavyopambana na tatizo la dawa za kulevya, ambalo limekuwa likipoteza nguvu kazi ya taifa.
Alisema dawa hizo zinachangia kurudisha nyuma maendeleo ya taifa huku vijana wengi wakiwa waathirika wakubwa.
Alibainisha kuwa, mapambano yaliyotangazwa na serikali ya awamu ya tano dhidi ya wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya, yanapaswa kuungwa mkono.
UVCCM YATOA TAMKO
UMOJA wa Vijana wa Chama ChaMapinduzi(UVCCM), umempongeza Rais Dk. John Magufuli, kwa hotuba aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge la 11 mjini Dodoma. Umesema hotuba ya Rais Dk. Magufuli licha ya kuwa na umakini, matarajio, matumaini, mwelekeo, dira na vipaumbele katika kuwatumikia wananchi, imeonyesha serikali yake ilivyopania kuimarisha huduma za jamii
UVCCM pia imesema hotuba hiyo imetoa dira ya maendeleo ya sekta ya utawala bora, haki na demokrasia, kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na uhusiano wa kimataifa.
“Dk. Magufuli katika hotuba yake, ameonyesha uwezo, kipaji na kipawa cha hali ya juu, ufahamu, dhamira na kusudio la kupambana na maadui ujinga, umasikini na maradhi,” imesema UVCCM.

No comments:
Post a Comment