KAMATAKAMATA ya vigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wanaotuhumiwa kuhusika na wizi wa makontena 349, imeendelea kushika kasi, baada ya vigogo wengine 12 wa TRA kutiwa mbaroni na polisi.
Wakati vigogo hao wakitiwa mbaroni, jeshi hilo limewataka vigogo wengine waliohusika na ubadhirifu huo kujisalimisha kabla hawajakumbwa na kamatakamata hiyo.
Kufuatia upelelezi unaoendelea kufanywa na maofi sa wa jeshi hilo waliobobea kwenye uhalifu dhidi ya makosa ya kifedha, watuhumiwa waliokamatwa ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru wa mamlaka hiyo, Tiagi Masamaki na Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru, Habibu Mponezya.
Wengine ni Eliachi Mrema ambaye ni Msimamizi wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha kwenye Bandari Kavu ya Kampuni ya Azam, Haroun Mpande kutoka Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta (ICT) na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara wa TRA, Hamis Omary.
Akizungumza jana, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani, alisema watuhumiwa wengine saba ambao bado jeshi hilo linawashikilia, majina yao hayajawekwa bayana kutokana na sababu za kiupelelezi.
“Majina ya watuhumiwa wengine yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi, lakini watuhumiwa watafi kishwa mahakamani mapema iwezekanavyo,” alisisitiza.
Kamishna huyo alisema, uchunguzi zaidi unaendelea kufanywa na jeshi hilo, hivyo watuhumiwa wengine waliohusika na wizi huo ni vyema wakajisalimisha kabla ya kukamatwa.
Kukamatwa kwa vigogo hao kumetokana na ziara ya kushitukiza kwenye Bandari ya Dar es Salaam, Novemba 27, mwaka huu, iliyofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Kwenye ziara hiyo, waziri mkuu alikutana na viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Bandari na TRA, ambako alibaini wizi wa makontena 349.
Kutokana na wizi huo, Majaliwa aliagiza polisi kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliohusikana na wizi huo wa makontena yenye thamani ya sh. bilioni 80.

No comments:
Post a Comment