Saturday 30 January 2016

KAZI YA RAIS MAGUFULI KUISUKA SERIKALI YA AWAMU YA TANO HAIJAKAMILIKA-SIMBACHAWENE


Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene, amesema kazi ya Rais Magufuli kuisuka serikali haijakamilika.

Amesema kazi hiyo kwa sasa inaendelea kwa wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi hadi kwa wakuu wa idara waliochujwa kuhakikisha wanaendana ya kauli mbiu yake ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Simbachawene alisema hayo juzi bungeni mjini Dodoma, wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia mjadala wa hotuba ya Rais ya ufunguzi wa Bunge. ìTanzania mpya ya Magufuli inayokuja ni ya watu wanaofanya kazi.

"Tunataka tuwahakikishie kwamba Rais anaendelea kuisuka serikali na mtambue kwamba serikali bado haijakamilika, bado tunahitaji wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya…tunakwenda vizuri zaidi tunataka kusuka wakurugenzi.

"Lakini tunakwenda mbali kusuka mpaka wakuu wa idara tunataka tuwachuje. Tunataka Tanzania mpya tukianzia juu tukisema ‘Hapa Kazi Tu’, basi ni kazi kweli," alisema Simbachawene.

Hata hivyo, alisema kumekuwa na mkanganyiko juu ya shule za bweni zilizojengwa na jamii kupitia mipango yao wenyewe ambayo haitambuliki na serikali ingawa inafahamu kwamba zipo hosteli za namna hiyo.

Shule hizo ni karibu 3,200 zenye watu 1,334,280 ni watoto wengi sana nafahamu hili huwezi kukurupuka kuja na mpango wa kuwalisha. Tumeona tuanze na hawa wa bweni, lakini baadaye kama itawezekana tunaweza kwenda na huko, lakini si jambo ambalo katika fungu hili la sasa tumejiwekea,î alifafanua.

Simbachawene aliwaomba wadau, wazazi na halmashauri ziendelee na utaratibu waliokuwa wakiutumia, lakini isitokane na maagizo ya shule kulazimisha wazazi.

Akifafanua zaidi juu ya mkanganyiko huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, alisema shule za bweni zina vigezo vyake ingawa zipo baadhi ya shule za kutwa zimejiwekea utaratibu wa hosteli japokuwa haziko kwenye utaratibu wa sasa wa wanafunzi kupata chakula.

Aliwataka wakurugenzi watendaji wa halmashauri nchini, kubaini kama kuna shule ilisajiliwa kuwa ya kutwa, lakini inakidhi vigezo iwe ya bweni, waende wizarani wabadilishiwe usajili.

No comments:

Post a Comment