Monday 30 May 2016

JK: VIJANA KUWENI HURU KUTOA MAONI, MKIKOSOLEWA JIREKEBISHENI



Na: Frank Shija, MAELEZO

Vijana nchini watakiwa kuwa huru kutoa maoni yao na wanapo kosea wawe tayari kukosolewa na kukujirekebisha.

Rai hiyo imetolewa na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne  Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya Pili ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika jana katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Kikwete alisema kuwa vijana wanapaswa kutoogopa kukosea, kwani watu hujifunza kutokana na makosa hivyo ni vyema wakathubutu kufanya mambo kwa kuzingatia misingi, weledi na kwa uwazi huku wakiepuka migawanyiko.

Wakati huo huo, Kikwete ameahidi kulisaidia Shirikisho hilo kanda na Dar es Salaam, jumla ya shilingi milioni 20, kwa ajili ya kusaidia katika kutekeleza mradi wao wa kilimo na ufugaji wa kuku.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM), Zainabu Abdallah alisema katika kuenzi na kutambua juhudi za Rais mstaafu Jakaya Kikwete katika kusaidia vijana, wataanzisha tuzo maalumu kwa vijana zitakazo julikana kama 'Jakaya Mrisho Kikwete Youth Awards'

Alisema lengo lake ni kuhamasisha viongozi waendelee kusthamini michango ya vijana katika kukuza na kuendeleza Taifa.

Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Seneta ya Dar es Salaam, linaundwa na jumla ya matawi 34, ambapo katika mahafali hayo ya pili, jumla ya wahitimu 640, walitunukiwa vyeti kutambua mchango wao katika kuimarisha uhai wa Chama vyuoni.

No comments:

Post a Comment