JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya
mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya
139.
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli
amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R.
Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.
Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia
amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith
Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar
es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais
Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F.
Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye
uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa
mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi
Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili
ya uongozi.
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya
139.
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia
mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya
miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru
sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali
itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo,
Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais
Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya
kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78
za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa
kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu
katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa
wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
1.
Arusha - Mrisho
Mashaka Gambo
2.
Arumeru - Alexander
Pastory Mnyeti
3.
Ngorongoro - Rashid Mfaume
Taka
4.
Longido - Daniel
Geofrey Chongolo
5.
Monduli - Idd Hassan
Kimanta
6.
Karatu - Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
1.
Kinondoni - Ally Hapi
2.
Ilala - Sophia
Mjema
3.
Temeke - Felix
Jackson Lyaviva
4.
Kigamboni - Hashim Shaibu
Mgandilwa
5.
Ubungo - Hamphrey
Polepole
DODOMA
1.
Chamwino - Vumilia
Justine Nyamoga
2.
Dodoma - Christina
Solomon Mndeme
3.
Chemba - Simon
Ezekiel Odunga
4.
Kondoa - Sezeria
Veneranda Makutta
5.
Bahi - Elizabeth
Simon
6.
Mpwapwa - Jabir Mussa
Shekimweli
7.
Kongwa - John
Ernest Palingo
GEITA
1.
Bukombe - Josephat
Maganga
2.
Mbogwe - Matha John
Mkupasi
3.
Nyang'wale - Hamim Buzohera
Gwiyama
4.
Geita - Herman
C. Kipufi
5.
Chato - Shaaban
Athuman Ntarambe
IRINGA
1.
Mufindi - Jamhuri
David William
2.
Kilolo - Asia
Juma Abdallah
3.
Iringa - Richard
Kasesela
KAGERA
1.
Biharamulo - Saada Abraham
Mallunde
2.
Karagwe - Geofrey
Muheluka Ayoub
3.
Muleba - Richard
Henry Ruyango
4.
Kyerwa - Col.
Shaban Ilangu Lissu
5.
Bukoba - Deodatus
Lucas Kinawilo
6.
Ngara - Lt.
Col. Michael M. Mtenjele
7.
Missenyi - Lt. Col
Denis F. Mwila
KATAVI
1.
Mlele - Rachiel
Stephano Kasanda
2.
Mpanda - Lilian
Charles Matinga
3.
Tanganyika - Saleh Mbwana
Mhando
KIGOMA
1.
Kigoma - Samsoni
Renard Anga
2.
Kasulu - Col. Martin Elia Mkisi
3.
Kakonko - Col. Hosea
Malonda Ndagala
4.
Uvinza - Mwanamvua Hoza Mlindoko
5.
Buhigwe - Col.
Elisha Marco Gagisti
6.
Kibondo - Luis Peter
Bura
KILIMANJARO
1.
Siha - Onesmo
Buswelu
2.
Moshi - Kippi
Warioba
3.
Mwanga - Aaron
Yeseya Mmbago
4.
Rombo - Fatma
Hassan Toufiq
5.
Hai - Gelasius Byakanwa
6.
Same - Rosemary
Senyamule Sitaki
LINDI
1.
Nachingwea - Rukia Akhibu
Muwango
2.
Ruangwa - Joseph
Joseph Mkirikiti
3.
Liwale - Sarah
Vicent Chiwamba
4.
Lindi - Shaibu
Issa Ndemanga
5.
Kilwa - Christopher
Emil Ngubiagai
MANYARA
1.
Babati - Raymond
H. Mushi
2.
Mbulu - Chelestion Simba M. Mofungu
3.
Hanang' - Sara
Msafiri Ally
4.
Kiteto - Tumaini
Benson Magessa
5.
Simanjiro - Zephania
Adriano Chaula
MARA
1.
Rorya - Simon
K. Chacha
2.
Serengeti - Emile Yotham
Ntakamulenga
3.
Bunda - Lydia Simeon Bupilipili
4.
Butiama - Anarose
Nyamubi
5.
Tarime - Glodious
Benard Luoga
6.
Musoma - Dkt. Vicent
Anney Naano
MBEYA
1.
Chunya - Rehema
Manase Madusa
2.
Kyela - Claudia
Undalusyege Kitta
3.
Mbeya - William Ntinika Paul
4.
Rungwe - Chalya
Julius Nyangidu
5.
Mbarali - Reuben
Ndiza Mfune
MOROGORO
1.
Gairo - Siriel
Shaid Mchembe
2.
Kilombero - James Mugendi
Ihunyo
3.
Mvomero - Mohamed Mussa
Utali
4.
Morogoro - Regina
Reginald Chonjo
5.
Ulanga - Kassema Jacob Joseph
6.
Kilosa - Adam
Idd Mgoyi
7.
Malinyi - Majula
Mateko Kasika
MTWARA
1.
Newala - Aziza
Ally Mangosongo
2.
Nanyumbu - Joakim Wangabo
3.
Mtwara - Dkt.
Khatibu Malimi Kazungu
4.
Masasi - Seleman Mzee Seleman
5.
Tandahimba - Sebastian M.
Walyuba
MWANZA
1.
Ilemela - Dkt.
Leonald Moses Massale
2.
Kwimba - Mhandisi
Mtemi Msafiri Simeon
3.
Sengerema - Emmanuel Enock
Kipole
4.
Nyamagana - Mary Tesha
Onesmo
5.
Magu - Hadija
Rashid Nyembo
6.
Ukerewe - Estomihn
Fransis Chang'ah
7.
Misungwi - Juma Sweda
NJOMBE
1.
Njombe - Ruth
Blasio Msafiri
2.
Ludewa - Andrea Axwesso Tsere
3.
Wanging'ombe - Ally
Mohamed Kassige
4.
Makete - Veronica Kessy
PWANI
1.
Bagamoyo - Alhaji Majid
Hemed Mwanga
2.
Mkuranga - Filberto H.
Sanga
3.
Rufiji - Juma
Abdallah Njwayo
4.
Mafia - Shaibu
Ahamed Nunduma
5.
Kibaha - Asumpter
Nsunju Mshama
6.
Kisarawe - Happyness
Seneda William
7.
Kibiti - Gulamu
Hussein Shaban Kifu
RUKWA
1.
Sumbawanga - Dkt. Khalfan
Boniface Haule
2.
Nkasi - Said
Mohamed Mtanda
3.
Kalambo - Julieth
Nkembanyi Binyura
RUVUMA
1.
Namtumbo - Luckness Adrian
Amlima
2.
Mbinga - Cosmas
Nyano Nshenye
3.
Nyasa - Isabera
Octava Chilumba
4.
Tunduru - Juma Homela
5.
Songea - Polet
Kamando Mgema
SHINYANGA
1.
Kishapu - Nyambonga
Daudi Taraba
2.
Kahama - Fadhili
Nkulu
3.
Shinyanga - Josephine
Rabby Matiro
SIMIYU
1.
Busega - Tano
Seif Mwera
2.
Maswa - Sefu Abdallah Shekalaghe
3.
Bariadi - Festo
Sheimu Kiswaga
4.
Meatu - Joseph
Elieza Chilongani
5.
Itilima - Benson
Salehe Kilangi
SINGIDA
1.
Mkalama - Jackson
Jonas Masako
2.
Manyoni - Mwembe
Idephonce Geofrey
3.
Singida - Elias
Choro John Tarimo
4.
Ikungi - Fikiri
Avias Said
5.
Iramba - Emmanuel
Jumanne Luhahula
SONGWE
1.
Songwe - Samwel
Jeremiah
2.
Ileje - Joseph
Modest Mkude
3.
Mbozi - Ally
Masoud Maswanya
4.
Momba - Juma Said
Irando
TABORA
1.
Nzega - Geofrey
William Ngudula
2.
Kaliua - Busalama
Abel Yeji
3.
Igunga - Mwaipopo John Gabriel
4.
Sikonge - Peres
Boniphace Magiri
5.
Tabora - Queen
Mwashinga Mlozi
6.
Urambo - Angelina
John Kwingwa
7.
Uyui - Gabriel
Simon Mnyele
TANGA
1.
Tanga - Thobias
Mwilapwa
2.
Muheza - Mhandisi
Mwanaisha Rajab Tumbo
3.
Mkinga - Yona
Lucas Maki
4.
Pangani - Zainab
Abdallah Issa
5.
Handeni - Godwin
Crydon Gondwe
6.
Korogwe - Robert
Gabriel
7.
Kilindi - Sauda Salum Mtondoo
8.
Lushoto - Januari
Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa
Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano
tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya
uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea
katika mikoa yao.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
26 Juni,
2016
No comments:
Post a Comment