KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdurahman Kinana amesema yupo tayari kufanya mazungumzo ya kuendelea na wadhifa wake huo endapo ataombwa na mwenyekiti mpya baada ya kuchaguliwa.
Kinana amesema binafsi alishatoa msimamo wake wa kutaka kung'atuka baada ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu uliopita, lakini akiombwa, atalazimika kuzungumza naye.
"Nilishasema awali kuwa nitang'atuka mara baada ya kukamilika uchaguzi mkuu na sasa wakati umefika, lakini mwenyekiti mpya akiniomba, tutafanya mazungumzo kama nilivyofanya mwaka 2012,'' amesema.
Kinana alisema hayo jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,
baada ya kutembelea ukumbi utakaotumika kwa ajili ya Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM.
Katibu Mkuu alisema amepata ujumbe wa simu za mkononi nyingi kutoka kwa watu mbalimbali baada ya kauli yake ya kung'atuka kuripotiwa kwenye gazeti la Uhuru, toleo la Julai 19, mwaka huu.
Aidha, Katibu Mkuu alisema kwa sasa yeye hana la kusema kama Chama kwani mambo mengi, ambayo Chama kilikuwa kikiyapigia kelele, serikali ya awamu ya tano inayafanyia kazi.
''Tulikuwa tunataka uwajibikaji wa serikali kwa wananchi wake, nalo linafanyika na matatizo mbalimbali ya wananchi yanatatuliwa, sasa sina la kusema, mambo yanaenda vizuri,'' alisema.
Akizungumzia maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, unaotarajiwa kufanyika keshokutwa mjini hapa, Kinana alisema yamekamilika na mkutano utafanyika kama ulivyopangwa.
Kinana alisema jumla ya mabalozi 23, kutoka nchi mbalimbali duniani wamethibitisha kuhudhuria mkutano huo, utakaofanyika kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Center (DCC).
Alisema mpaka sasa asilimia 90 ya wajumbe wa mkutano huo wameshathibitisha kufika mjini Dodoma na wanatarajiwa kuwasili kesho kwa njia ya mabasi na treni.
Katibu Mkuu alisema tayari magari ya kuwasafirisha wajumbe kutoka mikoani kuja Dodoma yameshatayarishwa kwa ajili ya kazi hiyo.
"Tayari wengi wa wajumbe wamethibitisha kuhudhuria mkutano na nina hakika kuwa wajumbe wote watapiga kura ya ndiyo kwa rais wetu kuwa mwenyekiti mpya,'' alisisitiza.

No comments:
Post a Comment