Friday 23 September 2016

MTOTO WA MIAKA SITA WA KIMAREKANI AMLIMA BARUA RAIS OBAMA



Picha ya Omran Daqdees mwenye miaka mitano ambayo alionekana akiwa na vumbi na damu baada ya nyumba yao huko Aleppo Syria kuharibiwa katika mlipuko, picha hiyo iliwashtua wengi duniani mwezi uliopita ikiwa ni pamoja na mvulana aitwaye Alex, ambaye anaishi Scarsdale, New York. Alex imembidi amwandikie barua President Obama ikiwa na mstari unaosema ‘atakuwa mwanafamilia mwenzetu na atakuwa kaka yetu’

Baada ya kupokea barua hiyo Rais Obama ameishare video kwenye ukurasa wake wa facebook  yenye barua hiyo na kuandika hivi…………
 
Alex ni mtoto mwenye miaka sita. Anaishi Scarsdale, New York Marekani, mwezi uliopita kama watu wengine duniani aliguswa na taarifa za picha za mtoto Omran Daqneesh, mwenye umri wa miaka mitano huko Aleppo Syria, aliyekuwa amekaa kwenye gari la wagonjwa (Ambulance) akiwa na taharuki huku akijaribu kujifuta damu mikononi mwake.
 
Hivyo Alex alikaa chini na kuniandikia barua, wiki hii katika mkutano wa Umoja wa mataifa uliokuwa ukijadili masuala ya wakimbizi, niliishirikisha dunia maneno mazito ya Alex.
 
Alex aliniambia alitaka Omran aende kuishi naye pamoja na familia yake, alitamani atumie naye baisikeli yake, pia amfundishe jinsi ya kuiendesha. Akasema dada yake atakuwa akimkusanyia vipepeo, na watakuwa wakicheza wote pamoja, akaandika “Tutamfanya familia na atakua kaka yetu.
 
Hayo ni maneno ya mtoto wa miaka sita ambaye bado hajajifunza kutuhumu au kuwa na wasiwasi na woga kwa watu wengine kulingana na walipotoka, wanavyoonekana ama jinsi wanavyo abudu.
 
Inabidi nasi  tuwe kama Alex, fikiria dunia ingekuwaje kama tungekua kama yeye. Tafakari tugepunguza maumivu kiasi gani na tungeokoa maisha ya watu wangapi. Msikilize Alex, soma barua yake, na ninafikiri utanielewa kwanini niliushirikisha ujumbe huu kwa dunia. 




No comments:

Post a Comment