Friday 25 November 2016

MBATIA AFANYIWA UASUAJI WA MGUU

MWENYEKITI wa NCCR-Mageuzi,  James Mbatia, amefanyiwa upasuaji wa mguu wa kushoto  nchini India.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Juju  Danda, alisema jana, kuwa hali ya kiongozi huyo  kwa  sasa inaendelea vizuri na afya yake inazidi kuimarika.

Alisema Mbatia alisafiri kwenda India, Novemba  10, mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa  mguu wake Novemba 14.

Danda alitaja sababu kubwa ya kufanyiwa upasuaji  wa mguu huo ni kutokana na matatizo aliyoyapata kipindi kilichopita wakati akiwa anacheza  mpira wa miguu.

Wakati huo huo,  Danda aliwataka wanasiasa nchini kuhakikisha  wanafuata sheria na  kuacha miemko ya  kisiasa ili  kulinda amani iliyopo.

Alisema amani ya nchi itaimarishwa  zaidi  kwa kudumisha umoja na mshikamano  bila kuangalia itikadi  za kisiasa  na kuhakikisha  maendeleo  yanapatikana.

"Changamoto kubwa ya kumaliza tatizo la rushwa na ufisadi ni mfumo wa ushughulikiaji uliopo, lakini  tunamuunga  mkono  Rais Dk. John Magufuli, kwa jitihada zake za kupambana na maadui hao," alisema.

Hata hivyo,  alisema  tatizo la  rushwa na ufisadi  nchini  halitaweza  kumalizwa na  mtu mmoja, bali  linahitaji ushirikiano wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment