Tuesday 15 November 2016

NACTE YAVIFUTIA USAJILI VYUO 26


BARAZA  la Taifa  la Elimu  ya Ufundi (NACTE), limevifutia  usajili vyuo  26, kwa  kushindwa kufuata taratibu  za usajili, ambapo vyuo 20 vimekuwa vikiendesha mafunzo bila ya kibali.

Aidha, vyuo viwili vimekuwa vikiendesha mafunzo katika vituo visivyosajiliwa na baraza hilo.

Baraza hilo limewagiza wamiliki wa vyuo hivyo, kuwatafutia wanafunzi wenye sifa vyuo vingine ama kuwarejeshea ada zao.

Kaimu  Katibu Mkuu  wa NACTE,  Dk. Adolf  Rutayunga, alitangaza uamuzi huo jana, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dar es es Salaam.

Alisema wamevichukulia hatua vyuo hivyo kwa kuvifutia usajili kutokana na kushindwa kuzingatia kanuni za usajili wa baraza hilo.

Dk. Rutayunga alivitaja vyuo hivyo kuwa ni Institute  of Managemment and Development  Studies (Iringa), Green Hill Instute (Mbeya),  Institute  of Business  and Social  Studies (Mbeya), Royal College  of Africa (Mbeya), Mbeya  Training  College,  Mbengwenya College of Bussness and Information  Technology (Mbinga).

Vyuo vingine ni New Focus  College (Mbeya), Shukrani  International  College  of  Busness  and Administration (Mbeya), Majority  Teachers College,  Rukwa  College of Health Sciences (Sumbawanga), Litembo Health  Laboratory Science School (Mbinga).

Pia vipo MAM Institute  of Education (Mbeya), Belvedere  Busness and Technology  College (Mwanza), Geita  Medical  Laboratory  Sciences  and Nursing Training College (Geita), Muleba Academy Institute (Muleba), St. Benard  Health  Training Institute (Geita), Victoria  Institute of Tourism  and Hotel  Management (Mwanza) na Gisan  Institute of Health  Science (Mwanza).

Kaimu Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa, vyuo vingine ambavyo vimekumbwa na sakata hilo ni Dar es Saalam Institute of Business Studies na Ellys Institute of Technology (Mara).

Vingine ni Tanzania Institute of Charted Secretaries and Administrators (Arusha), Emmanuel Community Institute (Kibaha), Modern Commercial Institute (Dar es Saalam) na Marian College of Law (Dar es Saalam).

Mbali na vyuo hivyo, Dk. Rutayunga alivitaja vyuo vingine, ambavyo vimekuwa vikiendesha mafunzo, ambayo hayajaidhinishwa na baraza hilo kuwa ni  Dar  es Salaan Institute  of Journalism and Mass Communication vya  Mwanza, Bukoba, Geita na Kahama.

Vyuo  vingine ni The Golden Training  Institute  Dar es Salaam (kozi ya  Certificate  in Sales  and Marketing,  Certificate  in  Record Management  and Certificate in Nursery  Teachers), Early  Childhood  Education na National Institute  of Agriculture  (Arusha).

Dk. Rutayuga alivitaja vyuo vingine kuwa ni Musoma Utalii Training  College (Musoma), Mwanza  Polytechnic cha Mwanza na  Maswa na  Nkurumah  Mkoba  Teachers College, kilichoko Kongwa mkoani Dodoma.

Alisema NACTE imevibaini vyuo viwili vinavyoendesha  mafunzo katika vituo, ambavyo havijapata kibali kuwa ni Mufindi Teachers College na  Rungembwa Teachers College, vyote  vya Mafinga.

Hivyo  NACTE imewataka wamiliki  wa vyuo,  ambavyo  havijakidhi masharti, kuhakikisha wanawatafutia vyuo vingine wanafunzi  walio na sifa  au kuwarudishia ada zao.

“Kwa wanafunzi wasio na sifa, walioko katika vyuo hivyo, mnapaswa  kuwarudishia ada zao au kuwapeleka shule  zinazowahusu,” alisisitiza.

No comments:

Post a Comment