Wednesday 8 February 2017

MANJI, AZZAN, MBOWE, GWAJIMA WATAJWA SAKATA LA WATUHUMIWA WA KUUZA DAWA ZA KULEVYA





Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji ni mmoja wa watu maarufu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, kuwa wanahitajika keshokutwa Ijumaa kwenye kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na madawa ya kulevya.

Makonda ametaja orodha ya majina kadhaa marufu kati ya 65 aliyodai kuwa anayo katika orodha yake ya wanaotakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya zoezi hilo la mahojiano katika kampeni yake ya kuendeleza kupambana na utumiaji na biashara ya madawa ya kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi zake leo jijini Dar, Makonda alimtaja Manji kuwa anatakiwa kufika kituoni hapo Ijumaa hii, pia alimtaja mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azzan ambaye alikuwa kipa wa timu ya wabunge na timu ya wabunge wa Simba wakati alipokuwa mbunge.

Majina mengine maarufu yaliyopo katika orodha hiyo ni na mfanyabiashara maarufu wa nguo, Hussein Pambakali, Mbunge wa Hai, Freeman Aikaely Mbowe, Mchungaji Josephat Gwajima.

Ameielezea orodha hiyo kuwa ni ya wale ambao wanahisishwa na biashara hiyo haramu na wengine wana taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara hiyo.

Watu hao watahojiwa na polisi kama ilivyofanyika kwa watu waliotajwa kwenye orodha ya kwanza iliyohusisha pia mastaa wa muziki na filamu.

Wengine wanaohitaji ni pamoja na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club.

Orodha ya awamu ya pili ya Makonda ina jumla ya majina 65.

No comments:

Post a Comment