Thursday, 7 September 2017

SIMBACHAWENE ABWAGA MANYANGA


ALIYEKUWA Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene Jana amejiuzulu wadhifa huo ili kupisha uchunguzi dhidi zinazomuhusu.

Simbachawene alitoa kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari Ofisini kwake na kusema akuwa yeye ataendelea kuwa mwaminifu kwa Serikali yake na anasubiria matokeo ya uchunguzi.

Alimshukuru Rais Dkt.John Magufuli kwa kumuamini katika  kipindi chote  na hivyo hana kinyongo chochote na mheshimiwa rais kwa maamuzi yake.

Alisema,kuwa katika ambadiliko yoyote lazima kuna watu wataumia na wengine watafurahia.

"Mimi siyo muhimu kuliko maslahi ya Nchi,hivyo nitabaki kuwa Mbunge Kama kawaida na nitawatumikia wananchi wangu "alisema Simbachawene

Hata hivyo aliwaomba wananchi wake wa Jimbo la Kibakwe kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho yeye ameamua kwa hiari yake kujiuzulu. Wadhifa wake.

Wakati huo huo naye aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Edwin Ngonyani alisema,ataandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake. 

No comments:

Post a Comment