Thursday, 7 September 2017

TUNDU LISSU ASHAMBULIWA KWA RISASI AKITOKA BUNGENI DODOMA



MBUNGE wa Singida Mashariki  Tundu Lissu Jana alishambiliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa katika gari lake eneo la Area D.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Dodoma ambaye pia ni mkuu wa mkoaJordan Rugimbana aliwaambia waandishi wa habari kuwa,tukio hilo limetokea jana majira ya saa saba mchana

Mbunge  huyo yupo hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma akipatiwa matibabu  na timu ya madaktari.

Rugimbana alisema Lissu amshambulia kwa risasi sehemu ya tumboni na mguuni na watu ambao hawaja Juliakana mpaka sasa.

Alisema watu hao wakiwa katika Nissan nyeupe walioshambuliwa lissu kisha kutokomea wasiojulikana

Alisema kwa mujibu aw taarifa za awali watu hao walikuwa weak ilifuatilia gali l Mbunge huyo kwa nyuma na waliporifikia walifuangua risasi.

 amewataka Wakazi wa Dodoma  kuwa watulivu wakisubiri taarifa rasmi ya jeshi la polisi na wakati huo huo kuzuia mikusanyiko ya watu katika maeneo mbalimbali ya Mji .

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa mkoa Dkt.James Charles alikiri kumpokea Lissu Mira ya saa Saba mchana.

Hata hivyo alisema Hali yake inaendelea vizuri akihudumiwa na jopo la madaktari Bingwa wa hospitali hiyo.

Naye Kamanda  wa polisi Mkoani Dodoma Gilles Moroto amewataka wananchi kutoa taarifa za watu waliofanya tukio hilo pindi watakapopata fununu za wahusika wa tukio hilo.

Alisema,tayari jeshi hilo limeshaanza msako wa kuwatafuta wahusika ikiwa ni pamoja na kufunga barabara zote zinazotoka nje ya mkoa.

No comments:

Post a Comment