Sunday 24 September 2017

VIKAO VYA CC, NEC KUFANYIKA DAR

VIKAO vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwemo cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vinatarajiwa kuanza kufanyika wiki hii.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyolewa jana na kutiwa saini na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, ilisema Kamati Kuu itakutana Septemba 27 na 28 mwaka huu.

Polepole alisema NEC itakutana kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vikao hivyo vitakaa kwa mujibu wa ratiba yake ya kawaida.

Alisema pamoja na mambo mengine, vikao hivyo vitakuwa na kazi ya kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho kwa wanachama wa CCM, walioomba uongozi katika ngazi ya wilaya.

No comments:

Post a Comment