Thursday, 3 September 2015

NEC KUWAWEZESHA WAOIGAKURA WALEMAVU


NA ATHNATH MKIRAMWENI
WALEMAVU wametakiwa kujitokeza kwa wingi kusikiliza sera za wagombea
na kushiriki kikamilifu uchaguzi mkuu, Oktoba 25, mwaka huu, ili
kuchagua viongozi wanaowataka.
Aidha wametakiwa kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo kipindi hiki
cha uchaguzi.
Mkuu wa Idara ya Uendeshaji Uchaguzi, Clothilde Komba, alisema hayo
jana na kuongeza kuwa NEC imejipanga kikamilifu kuhakikisha  walemavu
wanashiriki ipasavyo katika uchaguzi mkuu.
Alisema tume imewashirikisha walemavu na wakapendekeza kifaa cha
kupigia kura kwa wasiioona, kitakachotumika kupigia kura katika
uchaguzi.
Clothilde alisema kifaa hicho kitatumika kikiwa na maandishi ya nukta
nundu, kitakachomwezesha mtu asiyeona kupiga kura kumchagua kiongozi
anayemtaka.
Alisema kifaa hicho kitakapokamilika , wahusika watapewa elimu ya
jinsi ya kukitumia.
Imeelezwa kuwa watu wenye ulemavu wamefurahishwa na hatua ya tume
kusikiliza kilio chao.
Clothilde alisema kwa upande ya walemavu wengine, utaratibu utatumika
ule wa miaka yote ya kwenda kupiga kura, huku wakiwa na anayemwamini
kwamba atamtimizia mahitaji yake ipasavyo.

No comments:

Post a Comment