Aidha, Dk. Magufuli jana alidhihirisha kuwa ni mzee wa kazi na yuko ngangari
idara zote, pale alipopanda jukwaani na kuanza kupiga ‘push up’.
Tukio hilo lililoamsha
shangwe kila kona ya uwanja wa Kayanga, wilayani Karagwe, Dk. Magufuli
aliwaomba wananchi wamchague kwa sababu ana nguvu za kuendesha serikali makini
na hata kiafya yuko imara tofauti na wengine.
Akizungumzia zao la kahawa
akiwa wilayani Misenyi, katika Jimbo la Nkenge, Dk. Magufuli alisema kuuza kahawa nje ni kushindwa
kuimarisha uchumi wa ndani.
Alisema ili kuhakikisha bei ya kahawa inaongezeka, atapunguza kodi ambazo ziko 26.
Alisema kodi hizo ndizo zinazofanya bei ya kahawa kuwa chini, na anamini ikiwa juu, hata wafanyabiashara wa Uganda watafuata bidhaa hiyo Tanzania.
Kuhusu suala la vizuizi vilivyopo ofisi ya Mamlaka ya Mapato Misenyi, mgombea urais alisema atalitafutia ufumbuzi ili vikwazo hivyo viishe.

Fidia kwa wananchi
Kuhusu fidia kwa wananchi waliobomolewa nyumba kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege Misenyi, Dk Magufuli alisema atahakikisha wanaostahili kulipwa wanapata haki yao kwa mujibu wa sheria ya ardhi.
Aidha, alisema mgogoro wa ranchi unaendelea kufanyiwa kazi na Mkuu wa Mkoa, John Mongella na ana imani kubwa ufumbuzi wa haraka utapatikana na hakuna anayeonewa.
Aliahidi kujenga barabara kutoka Karagwe mpaka Benako yenye urefu wa kilomita 100.
Lakini, mgombea huyo aliwaomba wananchi wa Karagwe wamchague Innocent Bashungwa awe mbunge wa Karagwe.
Aliwataka wale wa Jimbo la Nkenge, wampe kura za kutosha Diodurus Kamara ili awe mbunge.
Aliendelea kuwakumbusha wananchi wa maeneo mbalimbali ya Kagera, kutowachagua viongozi wasio na kumbukumbu na wasio na uchungu na nchi.
Alisema hata shule za Kata zimejengwa na serikali ya CCM, lakini inashangaza kuona baadhi ya wanasiasa wa upinzani wakizipinga kwenye majukwaa.

Mbali ya kufanya mikutano
katika majimbo ya Karagwe na Misenyi, Dk. Magufuli alihutubia Kyerwa, ambako
alimuombea kura mgombea ubunge, Innocent Bilakwate.
Dk Magufuli, amemaliza majimbo tisa ya mkoa wa Kagera. Mengine ni Bukoba Mjini, Vijijini, Muleba Kusini na Muleba Kaskazini.

MSUKUMA AFUNGUKA TENA
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita,
Joseph Kasheku, maarufu kama Msukuma, amemponda Lowassa akiwataka wananchi kutomchagua
kwa kuwa hana sifa za uongozi.
Aidha, alifichua kuwa hata mikutano
yake ya kampeni ambayo amekuwa akiihutubia, hutanguliza fedha kwa ajili ya
kuwaandaa wananchi.
"Naomba niwaambie,
mimi ndiye najua siri kubwa za Lowassa… huwa wanatanguliza fedha kabla ya
kuanza kuhutubia,” alisema Msukuma.
Aliwataka wananchi kuendelea kuchukua fedha za mgombea huyo kwa kuwa ni sehemu ya zile zilizoporwa na mafisadi, hivyo hawana sababu ya kuziacha.

Hata hivyo, aliomba wananchi
kufanya uamuzi sahihi kwa kumchagua Dk. Magufuli kwani, ndiye anastahili kuwa
kiongozi wa nchi kutokana na uchapakazi wake.
Pia, aliwaponda wenyeviti wa zamani wa CCM, Mgana Msindai (Singida) na Khamis Mgeja (Shinyanga) kuwa ni makapi yasiyostahili kusikilizwa bali kupuuzwa.

Alimtaja Waziri wa zamani
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha kuwa naye ni mzigo na hana uwezo
kwenye siasa.
No comments:
Post a Comment