NA MOHAMMED ISSA, PEMBA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeweka historia ya aina yake kisiwani Pemba baada ya maelfu ya wananchi na wana-CCM kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
Mkutano huo ni wa kihistoria kufanyika jana, katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba.
Katika mkutano huo, umati mkubwa wa watu ulianza kujitokeza kuanzia saa 4:45, asubuhi na hadi kufikia saa 9:00 alasiri, eneo la viwanja hivyo lilikuwa limesheheni watu kiasi ambacho hadi sehemu ya kupita ilikosekana.
Wakiwa wamevalia fulana za njano na kijani huku wakiwa na picha mbalimbali za Dk. Shein, wananchi na wana-CCM muda wote walikuwa wakiimba nyimbo za Chama kwa staili ya aina yake.
Aidha, vikundi mbalimbali vya hamasa na burudani iliyokuwa ikitolewa uwanjani hapo, ilizidisha morali ya wananchi ambao muda wote walionekana wakiwa na furaha.
Baadhi ya wananchi na wana-CCM walikuwa wakipiga ngoma mithili ya 'mbwa kachoka,' ambayo ilionekana kuwavutia wengi na kutojali jua lililokuwa likipiga eneo hilo.
Mgombea urais wa Zanzibar, Rais Dk. Ali Mohammed Shein, alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, imetekelezwa kwa asilimia 90, visiwani humo.
Aidha, amewaonya wenye nia ya kutaka kufanya vurugu kuacha mara moja, vinginevyo serikali itapambana nao.
Dk. Shein alisema ameiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu, ambapo serikali yake imepata maendeleo makubwa.
Alisema amefanikiwa kuionggoza nchi kwa misingi ya amani, umoja na mshikamano na kwamba Zanzibar iko tulivu hivi sasa.
Dk. Shein alisema yoyote anayedhani kuwa anaweza kuleta fujo Zanzibar, atashughulikiwa kwa nguvu zote.
"Ninawasihi wasije wakafanya hivyo, nchi yetu iko salama atakayeleta fujo tutamshughulikia," alisema.
Alisema atawahudumia wananchi wa Zanzibar, bila ya kujali itikadi za vyama vyao.
Dk. Shein alisema mwaka 2010, uchumi ulikuwa asilimia 4.3 na sasa ni asilimia 7.2.
Alisema mfumuko wa bei umeshuka kwa asilimia kubwa na kwamba uchumi wa mtu mmoja mmoja umeimarika.
Dk. Shein alisema Zanzibar, hivi sasa inaelekea kwenye nchi zenye uchumi wa kati na ikifika mwaka 2020, lengo hilo litakuwa limefikiwa.
Kuhusu maeneo huru ya uwekezaji, alisema tayari mchakato huo umeanza na katika miaka mitano ijayo utakuwa umekamilika.
Alisema lengo la serikali ni kutoa ajira kwa vijana na tayari imeanza kujenga kituo cha wajasiriamali pamoja na kuanzisha mifuko ya wajasiriamali.
Dk. Shein aliwataka wananchi wasikubali kudanganywa na baadhi ya watu ambao wanadai, wakipata madaraka watatoa ajira kwa muda mfupi.
Alisema hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kumaliza tatizo la ajira kwa muda mfupi.
Mgombea huyo alisema serikali yake itaendelea kupambana na umasikini pamoja na kujenga viwanda vidogo ili wananchi wengi waweze kuajiriwa.
Alisema uamuzi wa kuinua zao la karafuu, ulikuwa umo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama, ndio maana hivi sasa kilo moja inanunuliwa kwa sh. 14,000, kutoka sh. 5000.
Dk. Shein alisema ni uongo anapotokea mtu na kudai uamuzi huo ni wa kwake.
Aidha, alisema serikali yake ilitoa miche ya mikarafuu kwa wananchi ili waweze kupanda mingi zaidi na kuimarisha zao hilo.
Dk. Shein alisema tani 5,340, za karafuu ziliuzwa nchi za nje hadi kufikia mwaka jana.
Akizungumzia suala la kupambana na magendo ya karafuu, alisema hivi sasa yameisha kwani serikali ilipambana vilivyo na suala hilo.
Dk. Shein alisema serikali yake imekarabati barabara zenye urefu wa zaidi ya kilomita 900.
Alisema barabara mpya zimejengwa Unguja na Pemba na kwamba, barabara kuu zote hivi sasa zimewekwa lami.
Dk. Shein alisema katika kipindi kifupi kijacho, barabara ya kutoka Chake Chake kwenda Wete, itaanza kukarabatiwa na kupanuliwa.
Aidha, alisema watajenga barabara zenye urefu wa kilomita 110, kwa Unguja na Pemba katika kipindi kifupi kijacho.
Kuhusu bandari, alisema serikali itajenga bandari mpya na ya kisasa, ambayo itakuwa na uwezo wa kushusha makontena 200,000, pamoja na kuijenga upya bandari ya Wete, Pemba.
Alisema Uwanja wa Ndege wa Karume, utajengwa upya na kuwa wa kisasa zaidi.
Dk. Shein alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ameboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuongeza mishahara.
Alisema kila idara ndani ya serikali yake, ina muundo wa utumishi ambao uliwekwa mahususi kwa ajili ya kuboresha maslahi ya watumishi.
Mgombea huyo alisema ataongeza kima cha mshahara ili wafanyakazi wafanyekazi zao vizuri bila ya uzembe.
Aliwataka wananchi wa Pemba kumchagua pamoja na Dk. Magufuli ili aweze kuwatumikia.
Dk. Shein aliwataka wananchi kuwachagua wabunge, wawakilishi na madiwani wa CCM.

BALOZI IDDI
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema mwaka huu, ndio mwisho wa Maalim Seif na kwamba urais atausikia kwenye redio tu.
Alisema Maalim Seif ni mtu mwenye uchu wa madaraka kwani mwaka 2010, alipoambiwa apeleke majina matatu ili jina mmoja liteuliwe kuwa makamu wa kwanza wa rais, alijipendekeza mwenyewe na hakupeleka majina mengine mawili.
Balozi Iddi alisema kutokana na uchu wa madaraka aliokuwa nao Malimu Seif angepata urais, asingeondoka tena madarakani.
Alisema mgombea huyo wa CUF, anawadanganya wananchi kuwa zao la karafuu amelipandisha yeye wakati limo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Huku akishangiliwa na umati uliojitokeza katika mkutano huo, Balozi Iddi alisema Maalim Seif hana uzoefu wa kuongoza nchi.
"Wenye uzoefu wa kuongoza serikali ni CCM na sio CUF, na tunamuhakikishia Maalim Seif kuwa mwaka huu ndio mwisho wake.
"Ataingia kwenye group (kundi) la wagombea urais walioshindwa katika kugombea urais mara nyingi kwani hii ni mara yake ya sita kugombea na zote ameshindwa," alisema.
Balozi Iddi alisema iwapo mwaka huu, Maalim Seif atashindwa na kukataa matokeo, Dk. Shein ataunda serikali pekee yake.
Alisema Maalim Seif amekuwa akilalamika kila anaposhindwa na kwamba mwaka huu, hawatamvumilia.

VUAI ALI VUAI
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alivitaka vyama vya siasa kufanya kampeni za kistarabu kama ilivyo CCM.
Alisema Chama kinasikitikishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya vyama vya siasa kuwatuma vijana kuchana picha za wagombea wa CCM.
Vuai alivitaka vyama hivyo, kufanya kampeni kwa amani na utulivu na kwamba CCM itaendelea kufanya kampeni zake kwa utulivu na ustaarabu.
Alisema Maalim Seif, hana uwezo wa kushinda katika uchaguzi wa mwaka huu na lazima atashindwa.

MOHAMED ABOUD
Akizungumza katika mkutano huo, mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM, Mohammed Aboud Mohammed, aliwataka wananchi kumchagua Dk. Shein kwani amefanya mambo mengi katika utawala wake.
Alisema katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Dk. Shein, Zanzibar imepiga hatua kubwa ya maendeleo na kwamba miaka mitano ijayo kutakuwa na maendeleo makubwa zaidi visiwani humo.
Mohammed alisema mabadiliko hayaji hivi hivi kama baadhi ya watu wanavyodhani na kwamba yanaletwa kutokana na mipango mizuri iliyowekwa na CCM.
Alisema mgombea mwenza wa CHADEMA, Juma Duni Haji, aliondoka chama cha CUF, kutokana na uchu wa madaraka na uroho wa fedha.
Mohammed alisema CUF imefika mwisho, baada ya Maalim Seif kung'ang'ania madaraka ndani ya chama hicho.
"Tokea mwaka 1995, hadi sasa anagombea yeye tu, hivi CUF hakuna mtu mwengine wa kugombea? Na hivi sasa Duni kakimbia na kujiunga CHADEMA, hivyo ni wazi kuwa chama hicho kimekufa," alisema.
Alisema CUF, inakwamisha maendeleo ya Zanzibar, kwani wawakilishi wake pamoja na mawaziri kutoka chama hicho, walisusia bajeti ya serikali mpaka ikanusuriwa na wawakilishi wa CCM, hivyo chama hicho hakina mapenzi na wananchi.

ALI KARUME
Akizungumza katika mkutano huo, mjumbe wa kamati ya ushindi wa Chama, Balozi Ali Karume, aliwataka wananchi wamchague Dk. Shein kutokana na uwezo mkubwa wa uongozi alionao.
"Dk. Shein anatosha, anatosha sana, ni kiongozi makini ambaye amefanya mambo mengi Zanzibar, hivyo kuna kila sababu ya kupewa ridhaa ya kuongoza nchi," alisema.
Alisema Dk. Shein ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa, ambaye katika uongozi wake ameifanya Zanzibar kupiga hatua kimaendeleo.
Kwa mujibu wa Balozi Karume, iwapo wananchi watachagua vyama vingine, watakaribisha masultani ambao watakuja kuchukua mashamba yao.
Bila ya kutaja jina la vyama hivyo, Balozi Karume, aliwataka wananchi wasijaribu kuchagua wapinzani kwani lengo lao ni kutaka kuleta masultani ambao wanakuja kuchukua mashamba ya karafuu.
MAUA ABEID DAFTARI
Dk. Maua Abeid Daftari, aliwataka wananchi kuichagua CCM pamoja na wagombea wake wote.
Akimzungumzia mgombea urais wa Zanzibar, alisema ni mchapakazi hodari ambaye amefanikiwa kunyanyua uchumi wa Zanzibar.
Dk. Maua alisema mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ni kiongozi makini na shupavu ambaye hana kashfa na kwamba ataweza kuliongoza taifa kwa salama na amani.
Katika mkutano huo, wasanii wa bendi ya Ya Moto na Peter Msechu, walikonga nyoyo za viongozi na wananchi waliohudhuria mkutano huo, baada ya kutoa burudani safi.

No comments:
Post a Comment