NA MWANDISHI WETU
KATIBU wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,
amesema mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa ni mchafu na kamwe hafai kuwa
rais.
Amesema mbali na Lowassa na wenzake ambao wamekimbia CCM
baada ya kukatwa kutokana na kukosa uadilifu, hana sifa za kuwa kiongozi na
hafanani na mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.
Nape, alipasua kuwa katika wizara zote alizowahi
kuziongoza, Lowassa alitia doa kwa kukosa uadilifu huku akijilimbikizia mali na
kusababisha changamoto kubwa kwa Watanzania.
Nape, alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, uliofanyika Uwanja
wa Mnazi Mmoja, mjini Lindi.
Alisema kukatwa kwa Lowassa kwenye mbio za kuwania uteuzi
ndani ya CCM,kulitokana na kuwa na makandokando mengi ikiwemo tuhuma za rushwa
na ufisadi.
“Tulimuondoa Lowassa kwa sababu kila nafasi aliyopewa
katika nchi hii alitumia vibaya madaraka yake, sasa huyo mtu anafaa kuwa rais?”
Alihoji Nape.
Alisema Lowassa alianza kutumia vibaya madaraka
alipokuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha Arusha, (AICC), Waziri wa
Mifugo, Waziri wa Ardhi na hata alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu, mambo yalikuwa
yale yale hadi akalazimishwa kujiuzulu.
“Huyu akiwa Waziri wa Mifugo alihamisha ng’ombe katika
ranchi za taifa na kujimilikisha kwa kuzihamishIa kwenye ranchi yake iliyoKo
mkoani Tanga.
“Lowassa hafai, ana ranchi kubwa, kachukua ng’ombe wetu
kawapeleka kwake na anawakagua kwa helikopta. Leo ndio anataka tumpe urais ili
afanye nini,” alihoji Nape huku akishangiliwa na umati wa watu uliofurika
kusikiliza sera za CCM.
Kuhusu mchakato wa kumpata mgombea urais, Nape alisema
Lowassa asipotoshe umma kuwa hakujadiliwa.
Alisema Lowassa alijadiliwa na wajumbe walitumia muda
mrefu kumjadili kabla ya kumuengua kwa kuwa hakuwa msafi na hafai kuwa rais wa
nchi.
“Nasema kwa niaba ya CCM, Lowassa hafai hata kidogo kuwa
rais kutokana na rekodi yake mbaya katika utendaji wa kazi. Nilimshangaa
akichukua fomu wakati ni mchafu.
“Naomba huyu babu anayejipitisha kwenu kuwa anataka
kwenda Ikulu, hafai hata kidogo na hata afya yake ina mgogoro, hata kunyanyua
mguu mmoja kucheza muziki jukwaani kama Dk. Magufuli hawezi,” alisema Nape.
Nape alitumia fursa hiyo kuonya kuwa CCM itashughulika
na vibaka wote walioandaliwa na UKAWA kufanya vurugu siku ya uchaguzi.
Huku akionekana kuchukizwa, Nape alisema wana taarifa kuwa
UKAWA wamejipanga kuvamia vituo vya wapigakura na kwamba, CCM haitakubali hilo
litokee, hivyo watakula sahani moja.
Pia, amemtaka Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye,
kuacha kuropoka katika majukwaa kwa kuisema vibaya serikali, vinginevyo
ataanika uchafu wake kwa Watanzania.
No comments:
Post a Comment