Monday, 14 September 2015

NGELEJA AZIUMIZA NGOME ZA UKAWA






NA PETER KATULANDA, SENGEREMA
KISHINDO cha uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa CCM katika jimbo la Sengerema, William Ngeleja, kimebomoa na kusambaratisha uongozi wa CHADEMA wa Kata na tawi la Katunguru, wilayani hapa.
Wakati kishindo hicho kikiangusha ‘nyumba’ ya UKAWA, Ngeleja amemtolea uvivu mgombea uraisi wa chama hicho, Edward Lowassa kuwa mbali ufisadi wa Richmond, alitaka kupiga dili jingine alipolidanganya taifa kuwa ataleta mvua ya mafuriko kutoka Thailand.
Chama hicho kilisambaratika juzi baada ya wanachama wake 46 wakiwemo vigogo wa Kata na Tawi la Katunguru kujiunga na CCM kwenye mkutano mkubwa wa Chama, uliofanyika Katunguru na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Kijiji hicho na maeneo jirani.

Dalili za kuwasambaratika kwa Chadema zilionekana wakati mgeni rasmi wa mkutano huo, Miraji Mtaturu ambaye ni Katibu wa CCM mkoani Mwanza, alipowapasha kuwa chama hicho kilisha uzwa na Mwenyekiti wake Freema Mbowe lakini watu walio na akili ndogo kama za kupe, bado wameng’ang’ania ‘peoples’.
Alisema, baada ya CCM kumtosa fisadi Edward Lowassa na kudakwa na Chadema, sasa hakizungumzii tena ajenda ya ufisadi, wamemtakasa fisadi na kumuona kama Lulu baada ya kuwanunua vigogo wa Chadema na washirika wao wa UKAWA.
Mtaturu alidai, akili za wapinzani hazioni maendeleo na wangekuwa wanapenda mabadiliko ya kweli wanaposhuka na Helkopta wangekuwa wanaacha michango ya saruji na bati kwa ajili ya ujenzi wa zahanati, shule na miradi mingine ya wananchi, badala yake huacha wamewatimulia vumbi.
“Iyenaaaa” ilianza Mtaturu aliposema “Santuri ya uongo ya Ukawa wameisikiliza mda mrefu na sasa wananchi wameichoka, Ukawa umekuwa sawa na ukahaba, umekuwa ulaghai, wawapuuze wapinzani na mumchague Dk John Magufuli ambaye atatuletea mapinduzi ya maendeleo na siyo tu mabadiliko,”

Ngeleja alipigilia msumari mwingine aliposema dili jingine la Waziri Mkuu huyo aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, alitaka kupiga dili jingine alipodanganya taifa kuwa ataleta mvua ya mafuriko kutoka Thailand ili tatizo la umeme liishe.
“Kila mtu anapenda sifa lakini Lowassa anazipenda zaidi ndiyo maana ni muongo, alilidanganya taifa kuwa ataenda kukodi mvua ya mafuriko kutoka Thailand ili tatizo la umeme liishe nchini, lakini ilishtukiwa…” alisema Ngeleja na kushangiliwa kwa kishindo, wafuasi 46 wa Chadema wakamiminika kurudisha kadi na kujiunga na CCM.
Walirudisha ni pamoja na Katibu na Mwenyekiti wa Chadema Kata na Tawi la Katunguru, Faida Nzeyele na Slyicus Magege ambao walisema wanakubaliana na Mtaturu kuwa Chadema kitakufa itakufa kwa sababu ya kuacha misingi yake ya kutetea wananchi na kuokota mafisadi.
“Mheshimiwa Katibu, kweli Chadema kitakufa maana sasa kimekuwa chama cha mafisadi, nasisi watu 46 tuliokuwa wanachama wake hatutaki kuwa na akili ndogo kama za kupe kung’ang’ania kwenye ngozi ya chadema ambayo imeisha liwa na Lowassa,” alisema Nzeyele na kuripua shangwe upya.

1 comment:

  1. Maneno ya wakosaji na hayana ukweli wowote tofauti na kutafta kiki tu! Pole zao wananchi wa mwaka 2010 sio walewale wameongeza upeo hatutaki propaganda za majukwaani tunataka tuone nikwa namna gani wawakilishi wametusaidia kuinua uchumi wetu! Sio kuoewa hela uandike kitu kisicho cha kweli.

    ReplyDelete