Thursday, 1 October 2015

MGOMBEA CCM ANUSURIKA KIFO




NA MIRIAM SARAKIKYA, ARUSHA
MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Imbasenyi kwa tiketi ya CCM, Ombeni Majenja (CCM), amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA.
Akizungumza na Uhuru jana, mgombea huyo alisema tukio hilo lilitokea Septemba 22, mwaka huu, saa 3:00 usiku, akiwa maeneo ya nyumbani kwake wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Alisema siku hiyo alikuwa akirejea nyumbani, lakini kabla ya kufika kwake, aliitwa na vijana wanne akiwa kwenye gari na ndipo aliposhuka ili kwenda kuwasikiliza.
Aliongeza kuwa badala ya kumwambia lolote, vijana hao walianza kumshambulia kwa matusi na kumpiga kabla ya kupata msaada kutoka kwa raia wema.
Majenja alisema walifanikisha kukamatwa kwa kijana mmoja na kumfikisha Kituo cha Polisi cha Usa River na kubaini walitumwa na mgombea udiwani wa CHADEMA, Gadieli Mwanda.

No comments:

Post a Comment